Na John Walter-Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini (Naibu Waziri wa Katiba na sheria) Paulina Gekul amegawa mitungi ya gesi 500 kwa Watendaji wa Mitaa na Mabalozi Ikiwa ni utekelezaji wa moja ya mipango ya serikali katika kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Awali Mheshimiwa Paulina Gekul aligawa mitungi 500 kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa na vijiji, hivyo ametoa Jumla ya mitungi 1,000 bure, Kutoka kampuni ya Orxy Energies.
Gekul amesema anatoa mitungi hiyo kwa Upendo Kutunza Mazingira kwa nguvu zote kama serikali inavyosisitiza ikiwa ni ahadi aliyowahi kuitoa na sio kwa ajili ya kuomba huruma kisiasa.
Mtungi mmoja wa gesi ya Orxy una thamani ya Shilingi 65,000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Pendo Mangali amempongeza Mbunge huyo kwa hatua aliyoanza kuichukua katika kukabiliana na uharibifu wa Mazingira kwa kugawa gesi hiyo ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa matumizi ya mkaa au kuni mjini Babati.
Pendo amesema Faida za kutumia nishati mbadala ni kuzuia uharibifu wa Mazingira unaosababishwa na uvunaji miti hovyo bila kufuata utaratibu.
Baada ya kukabidhiwa mitungi hiyo viongozi hao Mbalozi na Watendaji wa kata, mitaa na Vijiji, wamemshukuru Mbunge wao kwa kutekeleza ahadi yake huku wakiahidi kuendelea kufanya kazi ya kuelimisha jamii juu ya Umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda na kutunza Mazingira.