Mwalimu Irene Muro kutoka chuo cha VETA Moshi akielezea namna BIDHAA za chuma zinavyozalishwa na Chuo hicho Kwa mashine iliyoundwa chuoni hapo.
Mwalimu Irene Muro kutoka chuo cha VETA Moshi akielezea namna BIDHAA za chuma zinavyozalishwa na Chuo hicho Kwa mashine iliyoundwa chuoni hapo.
Mmoja wa wanafunzi Kutoka Chuo Cha VETA. Moshi ikiielezea mashine iliyoundwa chuoni hapo ili kuzalisha bidhaa za komeo za madirisha ya chuma na vipi yanayotumika sana Katika ujenzi wa Nyumba mkoani Kilimanjaro.
…………………………
SABASABA DAR ES SALAAM
Katika kuhakikisha kuwa Vijana wanaomaliza mafunzo ya Sfundi Stadi wanajikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira, Chuo cha VETA Moshi kimetengeneza Mashine inayounda zana ambazo zinatumika kuzalishia bidhaa kwaajili ajili ya viwandani.
Akielezea kuhusu Mashine hiyo, mwalimu Irene Muro kutoka chuo cha VETA Moshi, amesema Chuo chao kimebuni Mashine hiyo ili kuwaandaa wanafunzi wao kujiajiri pindi watakapohitimu mafunzo yao.
“Sisi tunamfundisha mwanafunzi kutengeneza zana ila tumeona maswali ni mengi kwamba unamfundisha mwanafunzi kuandaa zana za uzalishaji lakini anaenda kuzalisha kwa kutumia mashine zipi wakati mashine hazipatikani mtaani kwa urahisi?, Hivyo basi tukakaa na wanafunzi , tukawaekeza jinsi ya kutengenezea mashine ili kusudi akimaliza kusoma akiweza kutengeneza aweze pia kuwa na mashine yake mwenyewe.
“Mashine ijulikanayo kama ‘Eccentric Press Machine’ ambayo tumeitengeneza wenyewe walimu pamoja na wanafunzi kwa ajili ya kuzalishia zana mbalimbali za viwandani kama vile, Komeo, Bawaba, Sufuria, Sahani za Bati na bidhaa nyinginezo ” ameeleza Mwalimu Muro.
Ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kujiunga na vyuo vya VETA vilivyoenea kote nchini na kwamba, kwa kufanya hivyo watakuwa wamepiga hatua kubwa ya kujiajiri wenyewe na kumudu gharama za maisha.