Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenywa akishuhudia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROARDS Mohamed Besta kushoto na Zhu Chenhua Mwakilishi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya CGC kutoka China wakionesha mikataba ya ujenzi wa miradi ya BRT mara baada ya kusaini katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenywa akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba Mitano ya ujenzi wa BRT iiliyosainiwa Jijini Dar es salaam leo ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 500 ambayo imesainiwa na serikali kupitia wakala wa barabara TANROADS na Kampuni za ujenzi kutoka China na Tanzania.
………………………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mikataba mitano ikijumuisha mkataba wa ujenzi wa barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga kwa kiwango cha lami; sehemu ya Pangani hadi Mapinga, ambayo itagharimu zaidi ya shilingi Bilion 17. 86 kwa ufadhili wa serikali na Benki ya Dunia.
Miradi hiyo, minne ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa Mabasi Yaendayo haraka na Maboresho ya Barabara ya Morogoro Ubungo mpaka Kimara jijini Dar es Salaam miradi ambayo itagharimu jumla ya shilingi Bilioni 507.
Akizungumza leo tarehe 30/6/2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa utiaji saini, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema ujenzi wa barabara hizo zitasaidia kupunguza foleni pamoja na kutoa ajira kwa wananchi kipindi ujenzi utakapoanza.
Mhandisi Kasekenya amesema kuwa itasaidia kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji na kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Ujenzi ukikamilika utaondoa changamoto ya usafirishaji wa abiria na mizigo na kuongeza usalama pamoja na kukuza utalii katika Jiji la Dar es Salaam” amesema Mhandisi Kasekenya.
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mohamed Besta, amesema barabara ya TAMCO vikawe hadi pangani yenye urefu wa Km.13 ni kiungo kati ya Dar es salaaam na Kilimanjaro pamoja na Tanga.
Amesema kuwa katika utekelezaji wa ujenzi huo watajenga miundombinu ya kalakana kwa ajili ya kuoshea magari, sehemu ya matengenezo ya mabasi, ujenzi wa njia maalamu ya wapita kwa miguu pamoja kuweka kamera kwa usalama wa watumiaji.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenywa akishuhudia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROARDS Mohamed Besta kushoto akibadilishana mikataba na Zhu Chenhua Mwakilishi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya CGC kutoka China mara baada ya usaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa BRT jijini Dar es Salaam leo kwenye ukumbi wa Juliusi Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROARDS Mohamed Besta kulia akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka DART Dk. Eliud Mhede wakati wahafla ya utiai saini wamikatana hiyo.
Mbunge wa jimbola Kawe Mh. Dk. Josephat Gwajima kushoto na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Mharami Mkenge wakiwa katika hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo ya ujenzi wa mradi wa BRT.
Baadhi ya wakandarasi waliosaini mikataba hiyowakiwa pamoja na wataalam mbalimbali katika hafla hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROARDS Mohamed Besta akizungumza wakati akitoa maelezokabla ya kusainiana mikataba hiyo ya ujenzi.
Mbunge wa jimbo la Kawe Dk. Josephat Gwajima akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala na Mwakilishi waMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Edward Mpogolo akitoa salamu za mkoa wa Dar es Salaam katika hafla hiyo.