………………..
KAMPUNI Ya Uzalishaji wa mbolea Afrika (OCP) yazindua rasmi awamu ya tatu ya Mradi wa tathmini ya udongo ili kutoa elimu kwa wakulima juu ya aina za udongo na mazao rafiki kulimwa katika mikoa husika.
Akizungumza na Wanahabari Leo Juni 30,2023 Mkurugenzi wa Kampuni ya OCP Hillary Pato wakati akizindua Mradi huo amesema OCP ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo zaidi ya vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Musoma lengo likiwa ni Kuelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila ya gharama zozote kwa wakulima hao.
“Mradi huu wanufaika watakuwa wakulima zaidi ya vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Musoma ambapo kupitia mpango huo wa upimaji udongo ulioandaliwa na Serikali juu ya kutoa elimu kwa wakulima nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo ambapo kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa. “
Aidha Pato ameongeza kuwa Mradi huo wa upimaji na tathmini ya udongo unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 400 na kuwafikia wakulima wapatao 40,000 kufikia mwisho wa 2023.
Hata hivyo amesema Mradi huo tayari umewanufaisha Wakulima 39,0000 katika Nchi 08 bara la Afrika ikiwemo Naijeria,Togo, Ghana, Kenya,Burkina Faso,cote D’Ivoire na Senegal pamoja na nchi ya Tanzania kuwa Moja wa nchi wanufaika wa mradi huo.
Pia ametoa wito Kwa wakulima kuhakikisha wanakuwa na teknolojia za kisasa zitazowawezesha kuongeza uzalishaji wao na hivyo kuondokana na umasikini.
“Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo ni jambo la kipekee sana na hivyo tunahamasisha wakulima wote wawe sehemu ya mradi huu.”