Mkurugenzi Wa masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bw.Karimu Meshack akizungumza na mtandao wa Fullshangweblog katika banda la shirikahilo kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara ynayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wananci mbalimbali wakitembelea kwenyebanda la Shirika la Bima la Taifa NIC na kupata maelezo mbalimbali kuhusu huduma zao za bima wanazozitoa kwa wananchi.
Mkurugenzi Wa masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bw.Karimu Meshack akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake kwenye banda la shirika hilo katika maonesho ya biashara ya kimataifa ya viwanja vya sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
………………………………………..
Mkurugenzi Wa masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bw.Karimu Meshack ametoa wito kwa watanzania Kukata Bima za Mali , Ajali, Maisha na Kilimo ili Kujikinga na Majanga mbalimbali wakati yanapowatokea katika maisha yao.
Meshack amesema hayo wakati akizungumza na Fullshangwe katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kwenye Viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam,
Amesema kuwa asilimia 1.8 pekee ya watu nchini ndiyo waliojiunga na huduma za Bima hali inayoashiria Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu umuhimu Wa Bima.
Akizitaja Bima hizo na umuhimu wake ameitaja Bima ya maisha ambayo itawasaidia wanafamilia pindi mmojawapo atakapofariki ili kuendeleza maisha pasipo changamoto yeyote, Bima ya mali na ajali ,Bima ya uwekezaji fedha kidogokidogo ambayo itakuwa inampa Mwanachama faida ya asilimia 7 ya fedha anayoweka kila mwaka hii itamfanya mwanachama kuwa na akiba na fedha za uhakika katika kuendeleza Biashara Zake na maisha kwa ujumla.
Aidha Bw. Karimu ameeleza zaidi kuhusu Bima ya uwekezaji Kwa kutaja Gharama ya kujiunga kuwa ni shilingi elfu tano kwa mwezi kiasi ambacho Mtanzania yeyote anaimudu hivyo na unaweza kuweka kadri uwezavyo, amewataka wajasiriamali na wafanyakazi kujitokeza Kwa wingi kujiunga ili na Bima hiyo.
Aidha Bw.Karimu amesema Shirika la Bima linawajali wakulima na kuwataka kujiunga na Bima ya kilimo ili kumsaidia Mkulima dhidi ya Ukame,Mafuriko na Wanyama waharibifu wa mazao kwani Bima hiyo inalenga kumsaidia Mkulima alime pasipo kuwa na hofu kwa kufidia hasara yeyote atakayoipata katika shughuli zake zakilim.