Kamishna wa Elimu Nchini Lyabwene Mtahabwa amewataka Wazazi na Walezi kutokuwaachia walimu pekee suala la Malezi ya elimu ya Awali na Msingi ambayo ndio huanza kumjenga mtoto kiakili na Mwili.
Ameyasema hayo Mjini Morogoro wakati akifungua Mafunzo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa Wawezeshaji wa kitaifa wa Mafanzo ya Walimu wanaofundisha Wanafunzi wa Elimu ya Awali, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Boost.
Mafuunzo hayo ya siku Tatu analengo la kuwajengea uwezo walimu wa Awali Elfu Tatu kuwezesha ujifunzaji wa watoto wenye tija pamoja kuwawezesha Walimu kutumia vifaa vinavyopatikana Mazingira ya shule kufundishia.
Amesema licha ya kuwapeleka shule watoto kupata elimu pia wawape wasaha wa kujifunza maisha halisi ya kitanzania yatakayo wasaidia watoto uwelewa wa kutosha kuhusu Jamii yao kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo nchini.
Mratibu wa Mradi wa Boost kutoka TAMISEMI, Ally Swarehe amesema Wawezeshaji hao wanapata mafunzo ambayo yatawasaidia kuimarisha utendaji kazi wao pamoja na Walimu wengine ambao wataenda kuwawezesha.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetoa zaidi ya Bilioni 230 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu ya Awali na Msingi ikiwemo ujenzi wa madarasa maalumu ya mfano kwenye shule 302 zinazojengwa katika Halmashauri 184 kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa elimu ya Awali.
“Madarasa hayo yatakuwa na vifaa vilivyoboreshwa, wanafunzi kujifunza kwa ufanisi, lengo kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma kuanzia darasa la Awali hadi kidato cha nne” .Alisema Swarehe.
Swalehe amesema Mradi wa Boost umetengewa kiasi cha Sh Trilioni 1.15 ambazo zimeelekezwa kwenye sekta ya Elimu katika kuboresha elimu ya Awali na Msingi
BOOST ni Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji wa kwa shule za Msingi na Awali Tanzania Bara unaochangia Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 202526 ambao ni sehemu pia ya Lipa kulingana na Matokeo (EP4R).