Balozi wa China nchini Tanzania CHEN MINGJUAN akisaini makabidhiano ya magari 8 yenye thamani ya million 932 za kitanzania sawa na Dola laki nne za Marekani akiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Jumuiya ya EAC Ireni Isaka Kwa niaba ya katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwenye makao makuu ya EAC Jijini Arusha.
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
SERIKALI ya watu wa China imetoa Msaada wa magari 8 yenye thamani dola 400,000 Takribani million 932 za kutanzania pamoja na vipuri vyake kwa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki( EAC).
Aidha pamoja nakuleta wataalamu wa kutoa mafunzo ya matumizi ya magari na vipuri kwa madereva na mafundi wa Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki kwa ajili ya kuboresha shughuli za EAC.
Akiongea mara baada ya kukabidhi magari hayo Balozi wa China nchini Tanzania CHEN MINJUAN kwenye makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema kwamba zoezi hilo lilikuwa lifanyike mwaka 2021 lakini kutokana na janga la uviko ndio maana limefanyika mwaka huu.
Amesema serikali ya watu wa China imekuwa ikishirikiana na nchi za jumuiya ya Afrika mashariki katika masuala mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa miundombinu mbali mbali sanjari na kusaidia kukuza Demokrasia uwajibikaji na utawala bora.
“Tumekuwa tunasaidia katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kukuza Amani Demokrasia Utawala Bora na uwajibikaji utakaosaidia jamii ya watu wa Afrika Mashariki kupata huduma bora”
Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu mkuu EAC na Mkurugenzi wa sekta ya maendeleo ya Jamii, Irene Isaka amesema kwamba Jumuiya ya Afrika mashariki imekuwa ikishirikiana na serikali ya watu wa chini katika masuala mbalimbali ya kijamii katika kukuza mtangamano.
Alisema kwamba magari hayo yatasaidia shughuli mbali mbali za Kijamii katika mataifa 7 ya EAC ikiwemo matamasha ya vijana na wajasiriamali na sio kwa ajli ya ubebaji na shughuli za wa wafanyakazi wa jumuiya pekee.