***********************
Na Silvia Mchuruza.
Kagera.
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inamshikilia askali wa jeshi la wananchi Tanzania mwenye cheo cha Koplo(Corporal) aitwaye Nyambita Makayaga Magoma kwa kuomba rushwa.
Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa Takukuru mkoa John Joseph amesema kuwa askali huyo anashikiliwa kwa kosa la kuomba rushwa kwa mkazi mmoja wa wilaya ya Biharamulo kijiji cha Nemba Tsh. 3,000,000 kwa kosa la kuingiza ng’ombe katika hifadhi ya taifa(Biharamulo forest reserve.
Pamoja na hayo uchunguzi wa Takukuru ulibaini kuwa licha ya askali huyo kuomba kiasi hicho cha fedha Askali huyo alishikiliwa mifugo hiyo mpaka alipopatiwa jumla ya Tsh.800,000 na kisha kumwachia mwananchi huyo ambaye alilazimika kutoa taarifa hizo Takukuru.
Aidha ameongeza kuwa taasisi hiyo pia inamshikilia Koplo (Coplo) Nassoro Maulidy Mirambo kutoka kituo cha Runazi kwa kushilikiana na Bw. Asaph Manya Manya ambaye ni mwajiriwa katika Harmashauli ya wilaya ya Biharamulo idara ya misitu ambapo walishirikiana kumuomba rushwa mfanyabiashara wa mkaa mara baada ya kumkamata akiwa na maguni 50 ya mkaa.
Vilevile alisema kuwa uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba fedha hizo zilipokelewa na Bw.Nassor Maulidy Mirambo Agoust 23 mwaka huu kwa mikupuo miwili ambapo alipokea kwanza shilingi 250,000 kisha baadae akapokea kiasi cha Tsh.148,000 na baadae mfanyabiashara huyo aliweza kurudishiwa mkaa wake.
Sambamba na hayo mkuu wa takukuru mkoa alimalizia kwa kutoa lai kwa watumishi wa umma kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya rushwa vinginevyo watalipia kwa matendo yao wanayoyafanya.