Katika kuhakikisha vyanzo vya Maji vinalindwa na kuhifadhiwa, Jumuiya ya watumia Maji Ngerengere A na B imefanya uchunguzi Mkuu wa kupata viongozi wapya watakaosimamia Shughuli za Jumuiya hiyo.
Uchaguzi huo imefanyika Halmashauri ya Morogoro, Kata ya Ngerengere ambapo kupatikana kwa Uongozi Mpya wa Jumuiya ya watumia Maji Ngerengere utasaidia kutatua changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya Maji Mto Ngerengere.
Afisa Maendeleo ya jamii Mkuu, Bodi ya Maji Bonde la Wami – Ruvu Hhau Sarwatt amesema, mchakato wa viongozi umefanyika kwa mujibu wa mwongozo wa uundaji wa Jumuiya za Watumia Maji wa mwaka 2009.
“Lengo ni kuwashirikisha wananchi katika kupanga mpangoshirikishi wa usimamizi wa vyanzo vya Maji,kulinda,kutunza,kuhifadhi”. Alisema Sarwatt.
Amesema Jumuiya zimejumuisha watumia Maji ambao wamechukua Maji kutoka kwenye vyanzo vya Maji kwa kuweka miundombinu kwenye vyanzo vya Maji kwa matumizi mbalimbali ikiwemo Majumbani,Uanzishaji wa Nishati ya Umeme ,Kamati za umwagiliaji pamoja na ufugaji wa Samaki.
Jumuiya zimeundwa kwa Mujibu wa Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 na Sheria ya usimamizi wa Rasilimali za namba 11ya mwaka 2009.
Kwa Upande wao Viongozi waliochaguliwa wamesema watasimamia shughuli zote za Jumuiya Kwa weridi na kufuata miongozo iliyowekwa na Mamlaka husika bila ya kupendelea jamii moja.