Mratibu wa TASAF Manispaa ya Ilemela Leonard Nyamgenda akizungumza na wazee
…………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Halimashauri ya Manispaa ya Ilemela ni miongoni mwa wanufaika wa utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya Masikini TASAF awamu ya 3 na miradi ya kupunguza umaskini nchini.( TPRPV-OPEC.)
Kwa mujibu Wa Kaimu Mkurugenzi Wa Manispaa hiyo Sitta Singibala alieleza kuwa, tangu mwaka 2015 inanufaika na mpango huo ambapo hadi sasa Serikali imeshatoa kiasi cha sh. 7,837,874,786 kwa kaya masikini 5843.
Akizungumza wakati Wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi hiyo, Singibala alieleza kuwa Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na 2022/2023 halimashauri ilipokea kiasi cha Sh. 1,357,021,263 kwaajili ya kutekeleza miradi 21 ya kupunguza umaskini iliyofadhiliwa na OPEC.
“Tumefanikiwa kupata miradi 21 na kati ya hiyo, ni miradi sita pekee ambayo haijaanza utekelezaji wake na hii ni kutokana na changamoto za mfumo wa utoaji fedha wa Benki Kuu kutoruhusu fedha Kutoka.” Alisema Kaimu Mkurugenzi.
Alisema Pamoja na Changamoto hiyo, halimashauri imeweza kukamilisha Miradi mingine iliyobakia kwa asilimia 100 huku mingine ikibakiza asilimia chache kukamilika Ili iweze kutumiwa na walengwa.
Alifafanua kuwa Miradi 16 Kati ya 21 ni ya miundombinu(TI) ambayo thamani yake ni Sh. 1,097,444,728.09, miradi 12 inatekeleza Igogwe secondary kwa sh. 863,270,334.26, mingine mi 3 ipo katika kata ya Kitumba na itagharimu kiasi cha sh. 215,376,907.32, na mingine 2 ipo kata ya Sangabuye mtaa wa igalagala na kata ya Nyamhongolo mtaa Wa Ibinza.
Zuhura Mdungi ni Mkuu Wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano TASAF anaeleza kuwa, lengo la TASAF ni kuhakikisha kaya zisizo jiweza zinainuka na kuwa kaya bora lakini pia kuwa na miundombinu imara na ya kudumu kwenye jamii mbalimbali.
“Tumetembelea miradi mingi,inayofadhiriwa na TASAF na tumeona utekelezaji wake iko vizuri na tunaimani ambayo haijakamilika itakamilika kwa wakati na kwa ufanisi, na changamoto zilizopo zitatatuliwa” AlisemaZuhura.
Naye Mratibu wa TASAF Manispaa ya Ilemela Leonard Nyamgenda, ameeleza kuwa kwa sasa wanasubilia mfumo uruhusu kutoa fedha ili waweze kukamilisha na kuanza miradi mipya 6 iliyosalia.