Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe akiwa na kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo katika ziara Kata ya Zingiziwa kwa ajili ya kuakiki uhai wa Jumuiya ya Wazazi kuanzia ngazi ya Matawi na Mashina leo tarehe 22/6/2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe akizungumza jambo katika ziara ya kukagua Uhai wa Jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala wakizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi .
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Chanika wakiwa katika kikao kazi na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Zingiziwa wakiwa katika kikao kazi na Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe akigawa Kadi na kitini chenye mafunzo ya uongozi wa Jumuia ya Wazazi kwa viongozi wa matawi na shina.
Kamati Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Zingiziwa wakati wakikabidhi mifuko ya saruji 10 kwa ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Zingiziwa.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Lukooni, Kata ya Chanika Bw. Abdallah Pazi akizungumza jambo katika kikao kazi na Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Chanika wakitoa mapendekezo pamoja na kuwasilisha changamoto zao kwa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Bw. Mtiti Jirabi akisalimiana na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Zingiziwa.
……
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala imeendelea na ziara kwenda Kata kwa Kata kwa ajili ya kuakiki uhai wa Jumuiya ya Wazazi kwenye Matawi na Mashina.
Leo tarehe 22/6/2023 kamati ya utekelezaji imefika katika Jimbo la Ukonga Kata ya Zingiziwa na Chanika na kuzungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zilizopo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti akiwa katika Kata ya Chanika na Zingiziwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe, amewataka wanachama kuwa na umoja na ushirikiano jambo ambalo litasaidia kuleta tija katika jamii.
Mhe. Msofe amesema kuwa kila kiongozi kuanzia ngazi matawi na shina wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia nafasi ya uongozi aliyonayo.
Hata hivyo amewataka kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za Chama pamoja maisha yao.
Katika ziara hiyo kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala wametoa mifuko ya saruji 10 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Wazazi Kata ya Zingiziwa pamoja na kadi za Jumuiya ya Wazazi 50 kwa kila Kata.
Kamati ya Utekelezaji Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala itaendelea na ziara katika Kata ya Mzinga na Kitunda tarehe 23/6/2023