Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inashiriki Mafunzo na uingizaji wa taaifa zake katika Tovuti Kuu ya Serikali kwa lengo la kuhakikisha taarifa zote muhimu za Wizara na Taasisi zake zikiwemo huduma zinazotolewa (www.tanzania.qo.tz) kwa njia ya mtandao zinapatikana katika Tovuti Kuu ya Serikali ili kuwarahisishia wahitaji wa huduma hizo ndani na nje ya Tanzania kupata kwa urahisi bila kulazimika kufika katika ofisi husika.
Akiendesha mafunzo hayo Afisa Mawasiliano Mwandamizi eGA Bw. Rainer Budodi, amesema kuwa nidhamira ya Serikali kuhakikisha wananchi wa wadau mbalimbali wanapata taarifa muhimu za huduma na utekelezaji wa kazi za serikali kupitia Tovuti hiyo Kuu ya Serikali kwa kuziunganisha tovuti za Wizara na Taasisi zake, hivyo ni vyema washiriki wa Mafunzo hayo wakazingatia na kuhakikisha zoezi la kuingiza taarifa hizo linakuwa na ufanisi mkubwa.
Naye Afisa Habari Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Sixmund Begashe, licha ya kuipongeza Idara ya Habari- MAELEZO na Mamlaka ya Serikali ya Mtandao (eGA) kwa namna inavyo endesha mafunzo kwa utaalam wa hali ya juu, amesema mafunzo na zoezi hilo la Uwekaji wa Taarifa katika tovuti hiyo kuu ya Serikali ni daraja muhimu la kuisaidia umma kidijitali kuzielewa hudama zinazotolewa Serikalini.
Mafunzo hayo ya siku 3 ambayo yameandaliwa na ldara ya Habari – MAELEZO iliyo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali ya Mtandao (eGA), yanafanyika Jijini Mwanza yanaudhuriwa na Maafisa Habari kutoka Wizara mbalimbali nchini.