Viongozi wa dini wakiwa kwenye mkutano wa kawaida leo Juni 22, 2023 Jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kamati ya amani Mkoa wa Mwanza imeiyomba serikali kuendelea kutoa elimu na kuwaelimisha watanzania juu ya mkataba wa uwekezaji wa DP World baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai.
Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Juni 22, 2021 na Kamati hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya uwelewa wa wananchi kwenye mkataba huo katika ukumbi wa mikutano uliopo Vizano Hotel.
Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani Mkoa Askofu Charles Sekelwa ameeleza kuwa Dp World hawajawekeza Tanzania pekee, Bali wamewekeza katika Nchi nyingine kama Algeria, Angola, Djibouti, Misri, Msumbiji, Naigeria, Rwanda Senegal, Somaliland, na Afrika ya kusini.
“Kwa upande wetu sisi wananchi tuendelee kujadili jambo hili Kwa heshima na stara huku tukikumbuka na kutambua kuwa tayari jambo hili limekwisha pitishwa Bungeni na wawakilishi wetu” Alisema Sekelwa.
Aidha amewataka wanasiasa, viongozi wa dini kutojadili jambo hilo Kwa sura ya ukabila, udini, na ukada bali wajadili Kwa kuzingatia masilahi mapana ya Taifa.
“Jambo la muhimu kufahamu na kukumbuka Nchi yetu ya Tanzania huu sio uwekezaji wa kwanza kufanyika katika tawala tofauti kumekuwepo na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ndani ya Nchi yetu” Alisema Sekelwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani Mkoa Sheikh Hassan Kabeke ameeleza kuwa watanzania wamekuwa na Mikataba mingi ikiwemo ya ujenzi wa madaraja, ununuzi wa Ndege, pamoja na ujenzi wa Barabara haukuwahi kujadiliwa Bungeni.