Hamidu Said Diwani wa Kata ya Mirongo aliyepitishwa kuwa Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Diwani wa kata ya Mirongo Hamidu Said ameibuka kidedea katika uchaguzi wa Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya kupata kura14 kati ya kura 24.
Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatano Juni 21,2023 katika ukumbi wa ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana uliokuwa na wajumbe 24 kati ya 26 wanaoshiriki katika uchaguzi huku wawili hawakuweza kufika kutokana na majukumu na kinyang’anyiro hicho kuwa na wagombea watatu, Bhiku Kotecha, Hamidu Said pamoja na Charles Nyamasiriri.
Kura zilipigwa katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza Hamidu Said alipata kura 10 na Bhiku Kotecha kura 10 na Charles Nyamasiriri kura 4 na awamu ya pili iliweza kumuibua Hamidu Hamis kuwa mshindi Kwa kumzidi mpinzani wake kura 4.
Hamadi ameeleza kuwa pindi madiwani watakapompitisha kuwa Naibu Meya atahakikisha anashirikiana nao Kwa ukaribu pamoja na Mstahiki Meya kuhakikisha Halmashauri ya Jiji la Mwanza linafunguka Kwa watu wote wakiwemo wafanyabiashara.
Ameeleza kuwa atahakikisha anatenda haki Kwa Kila mmoja ili kuleta ustawi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kwa kufanya kazi Kwa ushirikiano.
Aidha amewataka watu wote waliopata dhamana ya kuwaongoza wananchi kuwatendea haki Kwa kufata Msingi na haki na kuhakikisha wananchi wanatatuliwa changamoto zao.
Msimamizi wa uchaguzi huo Jofrey Kavenga ameeleza kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki na Demokrasia Kwa Kila mgombea na kuwataka madiwani wote kufanya kazi Kwa umoja.
Kwa upande wao wagombea ambao kura hazikutosha wameeleza kuwa Kwa sasa wanapaswa kufanya kazi Kwa ushirikiano ili kuweka umoja na usawa na kuachana na makundi.
“Hapa hakuna mshindi sisi wote ni madiwani tuache makundi tukafanye kazi Kwa kutenda haki” Walisema.