Julieth Laizer, Arusha
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Dawa za kulevya duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa Juni 26 Jijini Arusha kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha,John Mongela,ameyasema hayo leo Juni 21 alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari na kueleza kuwa maandalizi yamekamilika ambapo maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonyesho yatakayofunguliwa Juni 23.
Amesema kuwa, kila mwaka madhimisho hayo ya kupiga vita matumizi ya Dawa za kulevya na dawa haramu huwa yanafanyika Kwa mjibu wa Azimio namba 42 la mwaka 1987 ambalo nchi yetu imeriridhia.
Amesema kuwa, mapambano dhidi ya Dawa za kulevya yanaigusa Jamii Kwa kuwa yanaathiri maendeleo ya Jamii na nguvu kazi.
Mongela amesema kuwa, matumizi ya Dawa za kulevya ni janga kubwa Kwa maendeleo ya taifa ambalo linapoteza nguvu kazi hivyo Kwa pamoja tupambane Kwa kuwa mwisho wote ni waathirika.
Ameongeza kuwa, katika mapambano hayo serikali imeanzisha vituo maalumu vya kuwasaidia vijana ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.