NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Ofis ya Makamu wa Rais na Muungano imefanikiwa kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo kupitia sera, kanuni mikakati pamoja na miongozo.
Akizungumza leo tarehe 19/6/ 2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Muungano Bw. Abdalla Mitanga, amesema kuwa mabadiliko ya tabia za nchi imeathiri sekta ya kijamii, uchumi pamoja na siasa.
Bw. Mitanga amesema Tanzania ni miongoni wa nchi zilizo athirika na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa isiyotabirika jambo ambalo sio rafiki kwa maendeleo ya Taifa.
“Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kutambua majukumu ya wahariri na waandishi wa habari nchini imeona ni vizuri kutoa elimu ambayo inakwenda kuelimisha jamii” amesema Bw. Mitanga
Amesema kuwa ili kufikia malengo serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikiratibu na kusimamia masuala ya uifadhi wa mazingira kwa kuratibu jitihada zinazofanywa za mataifa mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Amesema kuwa wadau wana jukumu la kusimamia utekelezaji wa kanuni na kufanya jitihada ambazo zimechukuliwa ili kutatua tatizo Hilo la uharibifu wa mazingira na kuifanya Dunia kuwa eneo salama Kwa maisha ya viunbe hai.