Wachezaji wa Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars wakishangilia goli baada ya kuichapa timu Taifa ya Niger goli 1-0 katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) Mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma akishangilia baada ya Timu ya Soka ya Tanzania Taifa Starts kuifunga goli Niger goli 1-0 katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) Mwaka 2023 nchini Ivory Coast
Mashabiki wa Timu ya Soka ya Tanzania Taifa Starts wakishangilia baada ya Timu yao kupata goli Katika mchezo wa Kutafuta nafasi ya kushiriki Mashindano Ya Mataifa Afrika (AFCON) katika mchezo uliopigwa leo tarehe 18/6/2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Na Eleuteri Mangi, WUSM Dar es Salaam
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeicharaza timu ya Niger goli 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Saimon Msuva mfungaji wa goli hilo ndiye shujaa wa mchezo huo uliochezwa Juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.
Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Wales Karia.
Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za mataifa ya Algeria, Niger na Uganda kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).