Kaimu Rasi wa ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Coretha Komba akizungumza jambo kabla ya mechi kati timu ya Wafanyakazi na timu ya Serikali ya wanafunzi (MUSO) leo juni 17, 2023, katika mchezo huo Wanafunzi waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Watumishi wa Ndaki ya Dar es Salaam kwenye Bonanza la michezo mbalimbali ambalo lina lengo la kuboresha afya ili waweze kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Coretha Komba akiwaongoza wafanyakazi na wanafunzi wa Ndaki hiyo katika kufanya mazoezi mbalimbali wakati wa Bonanza la michezo lilofanyika leo Juni 17, 2023 Katika viwanja Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta.
Mgeni rasmi katika Bonanza la Michezo Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba akikagua timu ya Wafanyakazi kabla ya mechi kuanza.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe akisalimiana na timu ya Wanafunzi kabla ya mechi kuanza.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Coretha Komba akiwaasa wachezaji wa timu zote mbili kucheza mchezo wenye amani na upendo.
Baadhi ya washiriki katika Bonanza wakicheza mchezo wa bao.
Washiriki wa Bonanza wakicheza Mchezo wa Drafti.
Mshindi wa kukimbiza kuku Bw. Daudi Mhehe akiwa ameshika kuku aliyeshinda wakati wa Bonanza la Michezo.
Washiriki wa Bonanza wakishiriki michezo mbalimbali.
………
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam pamoja na wanafunzi leo tarehe 17/6/2023 wameshiriki michezo mbalimbali ikiwemo kufukuza kuku, mpira wa miguu kupitia Bonanza la michezo ambalo limeandaliwa na uongozi wa chuo kwa ajili ya kutengeneza afya imara pamoja na kuwatia nguvu ya kufanya kazi kwa ufanisi.
Akizungumza wakati akifungua Bonanza la michezo lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe, Tegeta Ndaki ya Dar es Salaam, Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba, amesema kuwa michezo inaleta afya njema na kuifanya miili yetu kuwa katika mazingira mazuri.
Dkt. Komba amesema kuwa washiriki wa Bonanza wameshiriki michezo mingi yenye tija katika kuleta ufanisi.
Mratibu wa Bonanza, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Zitta Mnyanyi, amesema kuwa bonanza limeandaliwa kuwa ajili ya wafanyakazi katika kuhakikisha wanakuwa na afya njema.
Bi. Mnyanyi amesema kuwa Chuo kinasisitiza umuhimu wa michezo kwa ajili ya afya jambo ambalo litasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Tunashukuru uongozi wa chuo kwa kuwezesha kufanikisha bonanza la michezo, mwitikio umekuwa mkubwa kwa wafanyakazi” amesema Bi. Mnyanyi
“Katika mpira wa miguu timu ya wafanyakazi wa Chuo Cha Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam imefungwa magoli mawili kwa moja na wachezaji na timu ya serikali ya wanafunzi” amesema Bi. Mnyanyi.
Hata hivyo Chuo Kikuu Mzumbe kipo katika mkakati wa kuandaa ratiba ili kila jumamosi wafanyakazi washiriki mazoezi kwa ajili ya kuimalisha afya.