Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akimkabidhi Mwalimu Sophia Kagwerere kutoka Manispaa ya Arusha Mfano wa hundi ya shilingi milioni 3 mshindi wa jumla wakati wa kukabidhi Zawadi kwa Walimu Walioshiriki Shindano la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu Wa elimu ya awali kwenye ukumbi wa benki ya CRDB Upanga jijini Dar es Salaam.
……………………………
Walimu nchini wametakiwa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao jambo ambalo litasaidia kuwa na tija katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na uwelewa mzuri.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Zawadi kwa Walimu Walioshiriki Shindano la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu Wa elimu ya awali na Msingi Mkurugenzi Wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt.Aneth Komba amesema kuandaliwa Kwa Tuzo hizo ni kutia chachu Elimu kwani Zinasaidia kuwapa moyo Walimu Nchini Kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwapa Hamasa katika Ufundishaji mashuleni amesema kuwa wakati umefika kwa walimu kutumia ubunifu katika ufundishaji.
Dkt. Komba amesema kuwa kutumia mbinu za ufundishaji ni jambo rafiki ili kuhakikisha mtoto anapata wajibu wa kwenda Shule.
“Tuzo za mwaka huu zimezingatia namna bora ya ufundishaji ambao unajenga ustamilivu katika maisha” amesema Dkt. Komba.
Amefafanua kuwa uwasilishaji wa kazi kwa kila mwalimu zilitumika njia ya video ili kuhakikisha washindi wanapatikana.
“Tuzo za mwaka huu zimewalenga wa Walimu wa Shule ya awali na Msingi pamoja Hisabati” amesema Dkt. Komba
Tuzo za walimu ni Mradi umefadhiliwa na Benki ya Dunia na umelenga kuongeza uwezo wa walimu katika kufundishaji wa wanafunzi.
Aidha Dkt . Aneth amesema mbali na Tuzo zilizotolewa Leo Lengo kubwa ni kuboresha uwezo wa ufundishaji Kwa walimu,
walimu Wa awali na Wa masomo ya hisabati ili watoto wapende na kulielewa somo hilo .
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akimkabidhi Mwalimu Sophia Kagwerere kutoka Manispaa ya Arusha Ngao, Cheti na Mfano wa hundi ya shilingi milioni 3 mshindi wa jumla wakati wa kukabidhi Zawadi kwa Walimu Walioshiriki Shindano la Stadi za Ufundishaji kwa Walimu Wa elimu ya awali kwenye ukumbi wa benki ya CRDB Upanga jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Mkurugenzi Wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba kulia wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Sophia Kagwerere kutoka Manispaa ya Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zake.
Ofisa Mkuu wa Huduma za Benki ya CRDB BwBruce Mwile akikaidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 2.5 Mwalimu Jenipha Chuwa mara baada ya kuwa mmoja wwashindi wa shindano hilo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda na Mkurugenzi Wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba wakijadiliana jambo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo.
Waalimu waliofanikiwa kushinda wakishangilia kw furaha ushindi wao.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika hafla hiyo.
Bendi ya Mjomba Band ikitumiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba akizunguma katika hafla hiyo.