Wizara ya Madini inaungana na Wizara nyingine Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika kila tarehe 16-23 Juni ya kila Mwaka ambayo hubebwa na Kaulimbiu ya maadhimisho hayo.
Kaulimbiu ya Mwaka 2023 ni
Kufanikiwa kwa eneo huru la biashara Barani Afrika ( Acfta) kunahitaji Usimamizi wa Utumishi wa Umma wenye Mtazamo wa Kikanda.
Kufuatia maadhimisho hayo, watumishi wanasisitizwa kuzingatia maadili katika utumishi wa umma, utendaji ulio bora na kufanya vikao vya kujadili masuala mbalimbali ya utendaji wa Idara, Vitengo na Wizara kwa ujumla, kutoa maoni na kupokea ushauri.
Sambamba na maadhimisho hayo, Wizara inafanya maonesho ya shughuli mbalimbali zinazohusu Sekta ya Madini, Makao Makuu ya Wizara, Mtumba.