Katibu Tawala Wilaya ya Same Upendo Wella amewaomba watumishi na wadau mbali mbali Wilayani humo kumpa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuijenga nchi
Upendo ameyasema hayo wakati akikabidhiwa Ofisi na Katibu Tawala alihamishwa Sospeter Magonera ambaye amehamia Wilaya ya Hai.
Amesema ili Maendeleo yaweze kupatikana lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha katika kazi ambapo amewasisitizia Watumishi kuwa na umoja na upendo miongoni mwao.
“Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia Wananchi wa Same kwa kusimamia vema utekelezaji wa Miradi mbalimbali na kutatua Migogoro inapotokea katika Wilaya yetu,”Amesema Upendo Wella.