Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha,(IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika halfa hiyo Mkoani Kilimanjaro.
Viongozi mbalimbali wakishangilia ishara ya uzinduzi huo hafla iliyofanyika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Mkoani Kilimanjaro.
…….
Julieth Laizer ,Kilimanjaro..
Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kimesaini makubaliano ya ushirikiano rasmi ya uendeshaji wa kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo baina ya Jeshi la polisi (TPF) kupitia shule ya polisi Tanzania (TPS) Moshi .
Aidha utolewaje wa mafunzo hayo ni mojawapo ya mikakati ya kudhibiti wimbi la uhalifu mitandaoni kwa kuhakikisha wanatoka mafunzo kwa askari wake ili kukabiliana na vitendo hivyo.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo mkoani Kilimanjaro kati ya Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha ,Profesa Eliamani Sedoyeka baina yake na Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Camilius Wambura.
Wambura amesema kuwa , kupitia mafunzo hayo wanaenda kuboresha utendaji kazi katika maswala ya usalama wa mitandaoni katika jeshi la polisi kwani lazima wajengewe uwezo zaidi katika eneo hilo kutokana na kuwa ni uhalifu ambao umeshamiri sana kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hapa duniani .
Maeneo yetu sana katika dunia ya sasa hivi kuna mipango kikubwa inayofanywa katika uhalifu hivyo ni lazima wawe wamejipanga kwa kupata mafunzo mbalimbali namna ya kupambana na uhalifu.
“Dunia nzima imevamiwa na uhalifu huo kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hivyo baada ya kupata mafunzo hayo watakuwa wabobezi katika maeneo hayo ili waweze kupambana na wahalifu hao .”amesema.
IGP Wambura amesema kuwa ,makubaliano hayo ni muhimu sana kwa jeshi hilo kwani yatasaidia kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa jeshi hilo kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo hivi sasa.
Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) ,Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kuwa, mafunzo hayo yatafundishwa katika shule ya polisi na wakufunzi watatoka chuo cha uhasibu Arusha wakishirikianana wakufunzi wa chuo hicho cha polisi.
Ameongeza kuwa,kozi hizo zitaanza mwaka wa masomo ambao ni mwezi wa 10 na zitakuwa kozi nne tofauti,ambapo baada ya mafunzo hayo kutasaidia kudhibiti uhalifu mitandaoni kwani lazima tuwe na jeshi lenye wasomi linaloendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Profesa Sedoyeka ametaja kozi hizo kuwa ni Shahada ya sayansi katika usalama wa mitandao,Shahada ya sayansi katika usalama na masomo ya Kistratejia,Shahada ya uzamili katika masuala ya amani na usalama ,pamoja na Shahada ya Uzamili katika usalama wa taarifa.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi (SACP) ,Ramadhani Mungi amesema kuwa,kitendo cha kusaini makubaliano hayo yatawezesha jeshi la polisi kupata mafunzo ya kitaalamu ambayo yatawezesha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni kwani ili maafisa askari wawe weledi ni lazima wawe na mafunzo ya kutosha .
Ameongeza kuwa, watahakikisha makubaliano hayo yanaendelea vizuri na kuleta mafanikio ndani ya jeshi la polisi kwa ujumla kwani bila kuwepo kwa mafunzo hayo ya utendaji watakuwa na changamoto za hapa na pale.