Meneja wa kitengo cha maradhi yasioambukiza Zanzibar (NCD) Dkt.Omar Muhammed Sleiman akitoa taarifa ya matokeo ya zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi liliofanyika hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya afya wakati wa hafla ya kuwaaga timu ya madaktari kutoka China ambao walisimamia zoezi hilo huko Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.Juni 08,2023.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizumza na madaktari wa Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China ambao waliendesha zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi liliofanyika hivi karibuni katika vituo mbali mbali vya afya , wakati wa hafla ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwakabidhi vyeti vya ushiriki baadhi ya madaktari kutoka Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China ambao waloshiriki zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi liliofanyika hivi karibuni katika vituo mbali mbali vya afya , wakati wa hafla ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi cheti maalum Meneja wa kitengo cha maradhi yasioambukiza Zanzibar (NCD) Dkt.Omar Muhammed Sleiman wakati wa hafla ya kuwaaga madaktari kutoka Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China ambao waliendesha zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya Afya ,hafla iliyofanyika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.Juni 08,2023.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwakabidhi vyeti maalum watendaji wa Afya kitengo cha maradhi yasiambukiza walioshiriki zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi liliofanyika hivi karibuni katika vituo mbali mbali vya afya ,wakati wa hafla ya kuwaaga timu ya madktari kutoka Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China ambao waliongoza zoezi hilo,hafla iliyofanyika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.
…….
Na Rahma Khamis -Maelezo, Juni 08,2023
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka wananchi kuwahi Hospitali na kupatiwa tiba mapema ili kuepusha vifo visivyotarajiwa.
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazmmoja wakati alipokuwa akipokea taarifa ya matokea ya Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi uliofanyika hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya Afya Mjini na Vijijini.
Amesema kuwa maradhi hayo yameshamiri katika jamii hivyo ipo haja kwa wananchi kujitokeza mapema kufanya uchunguzi pindi zikitokea fursa kama hizo.
Aidha amesema kuwa amefurahi kuona maradhi hayo yanapatiwa matibabu Zanzibar hivyo watahakikisha vifaa tiba vinakuwepo katika kitengo cha maradhi hayo.
Waziri amesema Serikali ina nia ya kufanya kazi na Madaktari kutoka China ili wananchi wafanyiwe uchunguzi na kupatiwa matibabu ya uhakika.
Hata hivyo Waziri amewashukuru na kuwaomba madaktari hao kuendelea kuwa na ushirikiano kati yao na Serikali ya Zanzibar Kwani uhusiano wao unaleta tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa ya uchunguzi huo Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) Omar Mohamed Suleiman amefahamisha kuwa jumla ya akina 4412 wamefanyiwa uchunguzi ambapo kati yao wanawake 151 wamegundulika kuwa na tatizo hilo katika hatua tofauti.
Katika hatua nyengine Meneja amefahamisha kuwawaanawake 131 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo katika hatua za awali na wanawake 20 wamethibitika kuugua saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za juu ambapo hatua za matibabu zimeanza kuchukuliwa kwa wagonjwa hao.
ameongeza kuwa uchunguzi umebaini kuwa jumla ya wanawake 854 wamebainika kuwa na magonjwa mengine katika via vya uzazi ikiwemo magonjwa ya zinaa.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Amour Sleiman mohammed amesema Wizara inatumia gharama kubwa katika kuwapatia matibabu wagonjwa wa saratani hivyo kufanyika kwa zoezi hilo kumepunguza gharama za serikali kufanya matibabu hayo nje ya nchi.
aidha Ameishukuru timu ya madaktari kutoka Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China kwa ujio wao na kufanikisha kuwagundua wagonjwa wa tatizo hilo na kuwapatia matibabu.
hata hivyo mkurugenzi ameiomba timu ya madaktari hao kuongeza muda na awamu za kufanya uchunguzi ili kupunguza ongezeko la wagonjwa wa maradhi hayo.
itakumbukwa kuwa hivi karibuni timu ya madaktari kutoka Hospital ya Nanjing ya Jamuhuri ya watu wa China wakishirikiana na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha maradhi yasioambukiza waliendesha zoezi la uchunguzi wa Saratani ya shingo ya kizazi wakikadiria kufanya uchunguzi kwa wanawake 4000 na wamefanikiwa kuchunguza zaidi ya hao.