Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika futari iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wateja wake na wafanyakazi wa benki hiyo jana jioni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Katika futari hiyo pia watoto yatima kutoka moja ya kituo cha kulelea watoto wenye mazingira magumu na yatima Kigamboni walishiriki na kujumuika pamoja na wageni waalikwa kupata futari.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Ally Laay akikaribisha wageni waalikwa mbalimbali katika futari iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wateja wake na wafanyakazi wa benki hiyo jana jioni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akielezea malengo ya benki hiyo kwa wageni waalikwa mbalimbali katika futari iliyoandaliwa na benki ya hiyo kwa wateja wake na wafanyakazi jana jioni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Hamid Masud Jongo akitoa dua kwa ajili ya futari hiyo iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela wakiongoza wageni mbalimbali waalikwa kupata futari iliyoandaliwa kwenye hoteli ya Serena jana jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi Mstaafu wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akishiriki katika futari hiyo pamoja na wageni wengine waalikwa.
Wageni mbalimbali waalikwa wakijipatia futari.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Bw. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela wakipata futari pamoja na wageni waalikwa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaj, Waziri wa maliasili na Utalii Dk. Khamis Kigwangalla Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bw. Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nskela na Kamanda wa Polisi Mstaafu Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova wakizungumza mara baada ya kufuturu.