Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani.
Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam
……..
Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges inayomiliki hoteli za Kunduchi Beach, Embassy na Mikumi Wildlife Lodge imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri pamoja na kutengeneza mazingira rafiki baina ya serikali na wadau wa maendeleo ambao wamefanya uwekezaji nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail, amesema kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwa wafanya biashara nchini katika kuhakikisha wanafanya biashara katika mazingira rafiki.
Amesema kuwa kampuni yao inamilikiwa na watanzania wazawa kwa asilimia 100, huku wakimiliki miradi mingine kadhaa ya uwekezaji kutokana na mazingira mazuri yaliyopo nchini.
“Tunapenda kuwajulisha kuwa kupitia uwekezaji wetu sisi kama kundi la Wellworth tumeweza kutoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 525 na kuchangia pia pato la taifa kwa njia mbalimbali ,” amesema Ismail.
“Katika maono tuliyonayo ya kuzidi kuongeza fursa mwakani tutakuwa na hoteli 22 tumejipanga kuwekeza zaidi kwenye utalii ambapo hali ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutengeneza filamu ya Royal Tour serikali imetusaidia sana katika kupata idadi kubwa ya watalii kuja nchini,”amesema Ismail.
Ismail amezitaja hoteli zake hizo kuwa Gorogoro Oldean Mountain Lodge, Lake Manyara Kilimamoja Lodge,Tarangire Kuro Treetops Lodge,Ole serai Luxury Camp – Moru Kopjes, Ole serai Luxury Camp- Turner Springs, Ole serai Luxury Camp- Kogatende, Ole serai Luxury Camp- Seronera, Kunduchi Wet n Wild Waterpark.
Hoteli zingine ni Kinduchi Beach hotel, Zanzibar Beach resort, huku zilizokwenye ujenzi kwa sasa ni Serengeti Lake Magadi Lodge, Mikumi Wildlife Lodge na Zanzibar Whispering palms.
Mkurugenzi huyo amesema wameweza kupata “Booking” za wageni hadi wa mwaka 2025 ambapo kwa kazi wanazofanya katika nchi pamoja na upande wa utalii.
Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Josephine Makundi, amesema kwamba hotel na lodges zote za zinauwezo wa kuwahudumia wateja wanaolala zaidi ya elfu moja katika usiku mmoja.
Afisa Sheria na Utawala wa Kampuni hiyo Simoni Nguka, amesema kwamba
kuhusu umiliki wa Embassy Hotel Nguka kampuni hiyo ilinunua jengo la Embassy Hotel kutoka kwa kampuni ya Enterprise Tanzania Limited ambaye ndiye muuzaji wa jengo.
“Tulinunua jengo hili kutoka kwa muuzaji wa jengo na wala sio kutoka serikalini kwa utaratibu wa biashara ya kawaida ” free buyer na free saler ” na limenunuliwa baada ya kujiridhisha juu ya umiliki wake ambao haukutuonyesha uwepo wa serikali katika jengo hilo wala uwepo wao katika kampuni ya muuzaji ambao ndio waliokuwa wamiliki wa jengo kabla ya kuliuza kwetu”
Amesema kwamba baada ya kununua jengo walisajili mradi wa uwekezaji kupitia kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) nakupewa cheti cha usajili namba 031964 kilichotolewa 28/06/2013.
Hata hivyo wlikamilisha taratibu za kupata mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 23 kutoka katika benki mbalimbali lakini mikopo hiyo kwa sasa imefutwa baada ya mradi kukumbana na changamoto mbalimbali na kushindwa kuanza kwa wakati.
“Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa kesi Mahakamani baina ya waliokua wafanyakazi wa hotel hiyo na iliyokuwa menejimenti yao ( sio sisi) pia kesi baina yetu na muuzaji wa jengo kukiuka masharti ya mkataba, hivyo kesi hii bado inaendelea Mahakama ya rufaa.
Amesema kwamba waliinunua kutoka serikalini mwaka 1997 ambapo mpaka sasa ni miaka 26