Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said tarehe 2/6/2023 katika mkutano na viongozi wote wa Jumuiya hiyo kuanzia ngazi ya Kata na Matawi katika ziara ya kukagua uhai wa jumuiya katika Wilaya ya Ilala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe akifafanua jambo wakati akiongea na Walimu na Wazazi wa Shule ya Msingi Bunge akiwa katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said ya kukagua uhai wa Jumuiya pamoja na kutembelea Shule ya Msingi na Sekondari.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe akizungumza jambo na Katibu wa Jumuiya hiyo Bw. Mtiti Jirabi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Bw. Mtiti Jirabi akimkabidhi ripoti ya utendaji Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said katika Ofisi za Jumuiya hiyo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe akiwa na viongozi wa Kata ya Ilala pamoja na Wajumbe wa Kamati mbalimbali wakimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said.
Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM ngazi ya. Kata na Matawi wakiwa katika mkutano wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said.
…….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala imejipanga kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa vitendo ikiwemo kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi kuanzia ngazi ya Matawi na Kata jambo ambalo litasaidia kuendelea kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza tarehe 2/6/2023 jijini Dar es Salaam katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Khadija Said katika Wilaya ya Ilala, ambapo pia alizungumza na viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya matawi na kata, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe, amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa matawi ili kuleta tija katika utendaji.
Bw. Msofe amesema kuwa kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ni jambo rafiki ndani ya jumuiya na Chama cha CCM kwani ni muhimu katika kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama kupitia programu mbalimbali ikiwemo Mashindano ya Wazazi Cup.
Amesema kuwa katika ziara hiyo wamepokea maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi ngazi ya Mkoa katika kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri katika utendaji ikiwemo kuongeza hamasa ya kupata wanachama wapya wa jumuiya ya wazazi.
“Tunamshukuru Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa maelekezo mazuri ambayo ametoa na tunakwenda kuyafanyia kazi yote” amesema Bw. Msofe.
Amebainisha kuwa Bi. Said amefanikiwa kuwa kutembelea Shule ya Msingi Bunge pamoja na Shule ya Sekondari Mchanganyiko na kuzungumza walimu kuhusu muhimu wa kuwafundisha watoto maadili mema wakiwa shule, huku akisisitiza kuwa wazazi wanapaswa kutenga muda wa kuzungumza na vijana wao.
“Kila mwana CCM, jumuiya ya mzazi wawe mabalozi wazuri kuhusu maadili ya watoto kutokana kwa sasa kuna yamemong’onyoka wa maadili , wakina mama watenge muda wa kuzungumza na watoto pamoja na kuwakagua, wasikae mbali na vijana wao” amesema Bw. Msofe.
Hata hivyo amesema kuwa Mwenyekiti Bi. Said amewatambulisha wasimamizi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala ambao ni Bw. Salum Kibanda pamoja na Mwahamad Rahim ambao watakuwa na jukumu la kuhakikisha kila jambo linatekelezwa kulinagna na kanuni na utaratibu.
”Tunakwenda kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wasimamizi wa jumuiya ya wazazi katika wilaya ya ilala ambao wametambulishwa leo na Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam” amesema Bw. Msofe.