Kaimu Mtendaji Kijiji Cha Mgomba kati Flora Magoti akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Shule ya Sekondari Samia katika kijiji cha Mgomba Kati Mkoani Pwani wakati Watendaji kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Kamati ya kujitolea kusimamia Miradi ya TASAF Zanzibar CMC walipotembelea miradi hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgomba Kati wilayani Rufiji akifafanua jambo kwa Watendaji kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Kamati ya kujitolea kusimamia Miradi ya TASAF Zanzibar CMC wakati walipotembelea mradi wa ujenzi wa madarasa manne ya shule ya sekondari ya Samia.
Rose Ushaki Mkuu wa shule ya sekondari ya Samia iliyopo katika kijiji cha Mgomba wilayani Rufiji mkoani Pwani kwa Watendaji kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Kamati ya kujitolea kusimamia Miradi ya TASAF Zanzibar CMC wakati walipotembelea ujenzi wa shule hiyo.
Mwanajuma Musa Ali Mwenyekiti wa CMC Kizimkazi Dimbani Zanzibar akiuliza swali kutaka ufafanuazi kuhusu mambo mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa ujenzi wa shule hiyo ili kupata uzoefu wa usimamizi wa miradi kama hiyo Zanzibar.
Mwanafunzi Shaymaa Mohammed Ponela akiwasilisha maombi ya wanafunzi hao kwa selikali kuhusu Maji na Maabara ya shule yao ili kuwawekea mazingira mazuri ya kujisomea wawapo shuleni.
Wananfuzi wa Shule ya Sekondari ya Samia wakiwa katika picha ya pamoja.
Watendaji kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Kamati ya kujitolea kusimamia Miradi ya TASAF Zanzibar CMC wakati walipotembelea ujenzi wa shule hiyo.
Madarasa ya shule hiyo ambayo yamekamilika na yanatumiwa na wanafunzi.
……………………………………..
NA JOHN BUKUKU, KIBITI
Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imefanikiwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Samia yenye madarasa manne na matundu nane ya vyoo katika Kata ya Mgomba baada ya kupewa fedha Shillingi milioni 149, 675, 300 na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Shule ya Sekondari Mkoani Pwani,
Kaimu Mtendaji Kijiji Cha Mgomba kati Flora Magoti, amesema kuwa halmashauri
imepokea fedha za ujenzi kutoka TASAF
tarehe 15/9/2021 na kuanza utekelezaji wa mradi.
Amesema kuwa tarehe 27/ 9/ 2021 walianza ujenzi kwa kushirikiana wananchi kusafisha eneo la ujenzi.
Magoti amefafanua kuwa katika utekelezaji mradi huo wametumia mfumo wa (Force Account), huku akieleza kuwa gharama za ufundi ni Shilingi milioni 29, 937,000.
Amesema kuwa gharama za usimamizi wa ujenzi Shilingi million 16, 360, 610, ununuzi wa vifaa Shilingi 103,703, 420, na shillingi milioni 2,100,000 zimetumika katika kuchangia nguvu kazi ya wananchi.
“Ujenzi wa mradi huu umekamilika kwa asilimia 100 na wanafunzi tayari wameanza kutumia madarasa” amesema Magoti.
Ameeleza kuwa mwaka huu 2023 jumla ya wanafunzi 38 wakike wamepokelewa na wanaendelea na masomo katika Shule hiyo.
Amebainisha kuwa ujenzi wa Shule umekuja baada ya watoto wa kike kutembea umbali mrefu na kupata changamoto katika masomo yao.
“Miongoni mwa faida za mradi wa Shule kuondoa adha ya watoto wa kike kutembea umbali mrefu zaidi ya kilometa sita, kuongeza fursa za watoto wa kike kujiendeleza kielimu” amesema
Magoti.
Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji amesema kuwa madarasa hayo yatakuwa chachu ya maendeleo katika Kijiji cha Mgomba na Ikwiriri na Wilaya ya Rufiji.
Amesema kuwa Shule hiyo inakwenda kuzalisha wataalam hasa wasichana ambao ni watu muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.
Amesema kuwa ujenzi wa madarasa manne ni jambo kubwa kwao kwani watoto wengi watasoma katika Shule hiyo na kuleta maendeleo.
“Wapo Watendaji wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar pamoja na Kamati ya kujitolea kujenga miradi Zanzibar, kamati imekuja kujifunza namna ya kutekeleza miradi kwani Zanzibar kuna miradi mingi wanatarajia kutekeleza” amesema