Katibu wa Mbunge Dkt Angeline Mabula, Ndugu Kazungu Safari Idebe akikabidhi mabati Kwa viongozi wa tawi la Bupumula kata ya Nyamhongolo 7510: Katibu wa Mbunge Dkt Angeline Mabula Ndugu Kazungu Safari Idebe akihutubia wanachama wa CCM tawi la Bupumula kata ya Nyamhongolo hawapo pichani.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt. Angeline Mabula amechangia mabati kwaajili ya ujenzi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi tawi la Bupumula kata ya Nyamhongolo wilayani Ilemela
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Mbunge katika viwanja vya ofisi ya Serikali ya mtaa wa Bupumula, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Ndugu Kazungu Safari Idebe amesema kuwa Mbunge amekuwa akichangia fedha taslimu, matofali, mabati na vifaa mbalimbali katika miradi ya chama na Serikali ili kurahisisha huduma kwa wananchi
“Hii si mara ya kwanza mbunge wetu kuunga mkono juhudi za wanachama wa CCM na wananchi, Wakati ujenzi wa ofisi hii unaanza alitoa tofali na leo amekabidhi mabati lengo ni kufanya chama kuwa na sehemu yake kwaajili ya kufanya shughuli zake za kila siku bila usumbufu wowote,” alisema
Aidha Ndugu Kazungu amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa fedha anazotoa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwaasa wananchi kumuombea na kumuunga mkono
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi huo, Katibu wa CCM tawi la Bupumula Ndugu Joshua Mahenga amefafanua kuwa ujenzi wa ofisi za tawi hilo umefadhiriwa kwa kiasi kikubwa na Mbunge huyo hivyo kuwaomba wadau wengine na wanachama kujitoa na kuchangia kama sehemu ya kuunga mkono juhudi hizo
Nae Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nyamhongolo Mhe. Izengo Nkenguye mbali na kumpongeza Mbunge Dkt. Angeline Mabula Kwa kazi nzuri anazozifanya amewahakikishia ushindi wa CCM wanachama waliohudhuria mkutano huo kwa nafasi za uchaguzi wa Serikali za mitaa, udiwani, ubunge na Urais
Anna Sebastian ni mwanachama wa CCM kutoka kata ya Nyamhongolo amewaasa viongozi wengine kuiga mfano wa Mbunge Dkt. Angeline Mabula katika kuchangia, kusimamia, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo unaochochea maendeleo katika maeneo yao