Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani akikata utepe wakati akizindua Ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 676 – 300F ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam (PICHA IKULU/ JOHN BUKUKU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Makumu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakiwasili katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kushiriki hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 – 300 F yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja iliyofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam.
Maelfu ya wananch wakiwa katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja iliyofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam itakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Makumu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Mjaliwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi, Katibu wa NEC, Itikadi wa Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Sophia Edward Mjema wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 – 300 F yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja iliyofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani akipanda katika ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 – 300 F yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa kwenye Chumba cha Marubani ya Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL mara baada ya kuizindua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3/6/ 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mama Mariam Mwinyi mara baada ya kuzindua Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3/6/ 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akishuka kwenye Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3/6/2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mmoja wa Marubani walioileta Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Kapteni Neema Swai mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3/6 /2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Marubani walioileta Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Captain Neema Swai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalumu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3 /6/ 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalumu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 3 / 6 /2023
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amewataka watanzania kuendelea kuwaombea mema viongozi wa serikali ili wapate nguvu ya kufanya maendeleo ya nchi.
Akizungumzia leo tarehe 3/6/2023
katika Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
jijini Dar es Salaam katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 676 – 300F, Mhe. Dkt. Samia, amewaomba watanzania kuendelea kuwa pamoja na serikali katika kufanya shughuli za maendeleo.
“Naomba tuendelee kuwa pamoja nasi , tuombeeni tupate nguvu, tufanye kazi tupate mapato, tumeombwa ndege nyengine ya mizigo tunalifanyia kazi” amesema Rais Mhe. Dkt. Samia.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa Wizara ya ujenzi inatambua serikali imekuwa kitoa kipaombele katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Profesa Mbarawa amesema kuwa wataendelea kusimamia uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ili miradi hiyo isawaidie watanzania katika kuboresha maisha yao.
Amesema kuwa ujio wa ndege ya mizigo unakwenda kuwa chachu kwa wafanyabiashara wa wanatanzia na nchi mbalimbali.
“Wizara itaendelea kutekeleza lengo lake kuu la kuandaa sera zitakazosaidia usimamizi wa rasilimali zinazofanywa na serikali ili kuleta matokeo makubwa katika ukuaji wa uchumi nchini” amesema Profesa Mbarawa.
Amesema kuwa Wizara itaendelea kujenga mazingira wezeshe ya uchumi katika sekta binafsi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
Profesa Mbarawa amefafanua kuwa sekta ya usafirishaji inaleta uhai katika uchumi, hivyo wataendelea kushirikiana na sekta nyengine zinazozalisha mizigo katika kuhakikisha wanafikisha maeneo mbalimbali duniani.
“Wizara ya ujenzi itaendelea kuiboresha miundombinu ya viwanja mbalimbali vya ndege ili kuwezesha mashirika ya ndege ndani na nje kwa kutoa huduma kwa ufanisi zaidi” amesema Profesa Mbarawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, amesema kuwa Kampuni ya Ndege ya ATCL katika kutekeleza mpango wake wa pili wa miaka mitano kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 hadi 2026/2027 inatakiwa kuwa na ndege 20 ikiwemo ndege ya masafa mafupi 8.
Ameeleza kuwa kuwa ndege ya masafa ya kati zitakuwa 8, masafa marefu 3 pamoja ndege moja kubwa mizigo.
“Mapokezi ya ndege hii inaifanya ATCL kuwa na ndege 13 zilizopo, ndege tatu zinaendelea kuundwa, ndege mbili zinatarajiwa kuwasili nchini mwaka huu na nyengine mwaka 2024” amesema Matindi.
Amesema kuwa kutokana na uhitaji ni vyema ndege za mizigo zikawa mbili “Mhe. Rais tunaleta ombi letu kwako, utuongezee ndege moja ya mizigo ili kukabiliana na uhitaji wa soko”
Amesema kuwa mpango wa kununua ndege za mizigo umelenga usafirishaji wa bidhaa kutoka na kuingia pamoja na kuongeza thamani za bidhaa ili kuleta ushindani katika soko la Kimataifa.
Hata hivyo Matindi amesema kuwa ujio wa ndege ya mizigo inaiwezesha ATCL na kuifanya Tanzania kupata fursa ya kusafirisha mizigo kwenda nchi mbalimbali.
Amesema kuwa mizigo hiyo ni minofu ya samaki kutoka kanda ya ziwa, dagaa kutoka na samaki wa mapambo kutoka ziwa Victoria, nyama kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, kaskazini pamoja na katikati ya nchi.
Mizingo mingine ni maua, matunda na mboga mboga kutoka Mikoa ya kaskazini mwa nchi pamoja na mazao ya baharini kutoka Zanzibar na maeneo mengine kutoka ukanda wa bahari ya hindi.
“Mazao hayo yanaharibika haraka hivyo tukitumia usafiri wa anga ni rafiki katika kuhakikisha bidhaa inafika kwa haraka sokoni” amesema Matindi.
Ndege ya mizigo aina ya Boeing 767 ina uwezo wa kubebe mizigo hadi tani 54 kwa safari moja na inakwenda kuondoa adha ya wafanyabiashara waliokuwa wakipeleka mizigo yao nje ya nchi kwa ajili ya kusafirisha.
Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wameonekana kuwa na furaha kubwa kutokana Tanzania imeandika historia ya kununua ndege mizigo yenye uwezo wa kukaa angani saa 10.