Maelfu ya wananch wakiwa katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam itakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Hassan Suruhu (Picha na John Bukuku)
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakiwa katika picha ya pamoja leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda pamoja na Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Dorothy Kilave wakiwa katika picha ya pamoja leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yahendayo Haraka (DART) Dr. Edwin Mhede katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Kuwezesha Wanawake ngazi ya Taifa Bi. Fatuma Kange akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumtunza Mwimbaji wa Nyimbo za Taarabu nchini Bi. Hadija Kopa katika hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 yenye uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja inayofanyika katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 3/6/2023 jijini Dar es Salaam.
Mhubiri wa Kanisa la Inuka Uangaze Boniface Mwamposa ni miongoni mwa viongozi wa dini watakaoshudia ujio wa ndege ya mpya ya mizigo.
……….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Maelfu ya Wananchi wamejitokeza katika Viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kuungana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani katika mapokezi ya ndege mpya ya mizigo ya aina ya Boeing 767.
Ndege ya mizigo aina ya Boeing 767 ina uwezo wa kubebe mizigo hadi tani 54 kwa safari moja na inakwenda kuondoa adha ya wafanyabiashara waliokuwa wakipeleka mizigo yao nje ya nchi kwa ajili ya kusafirisha.
Ujio wa ndege ya mzigo itasadia kukuza uchumi wa mchi na kufungua milango katika soko ikiwemo China na India na masoko makubwa yanayozunguka yanayotegemea bandari ya Tanzania kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Zimbabwe na Comoro.
Uwekezaji huu umekuja wakati mwafaka kipindi ambacho Serikali ya awamu ya sita imejikita katika ukuaji wa uchlukiangalia ukuaji wa GDP (pato la ndani) unakwenda vizuri, ukiangali uwekezaji unakwenda vizuri, pia ukiangalia imani ya watu hususani wawekezaji imekuwa nzuri.
Kupitia uwekezaji huo unaofanywa na Serikali Shirika la ndege Tanzania (ATCL) unalenga kukuza uchumi wa Tanzania.
Machi 20, 2023 Mkurugenzi wa ATCL alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Ladislaus Matindi amesema “Tumekuwa tukitumia ndege za abiria, sasa kidogo ina changamoto kwa sababu haitupi nafasi ya kutosha kusafirisha mizigo”
“Lakini baada ya kupata ndege maalum ya kusafirisha mizigo itakayokuja mwanzoni au mwishoni mwa mwezi ujao aina ya Boing 767 itatatua changamoto hii,” amesema.
“Tumeona watu wasikilize changamoto zetu, tunasafirishaje, changamoto ni zipi? Ili tuhakikishe mizigo iliyokuwa ikipitia nchi nyingine isafirishwe moja kwa moja kutoka Tanzania.
“Mwaka uliopita tumesafirisha tani 2,600, hilo ni ongezeko kubwa maana tulipoanza mwaka 2017 tulikuwa tunasafirisha tani 350 hivi, tunahakika kwa mwaka huu tutakwenda zaidi ya tani 3000,” amesema.
“Tunashukuru Serikali imesikia kilio chetu na inaleta ndege ya mizigo, tunategemea kuitumia kwa sababu itatoa suluhisho,” amesema