Wazazi na walezi,wameshauriwa kuwasomesha watoto wao kwenye shule zenye miundombinu bora ya elimu ambayo itasaidia watoto wao kupata elimu bora itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.
Mdau wa elimu,ambae pia ni Diwani wa kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,Seifu Chomoka ametoa rai hiyo mei 31 nwaka huu wakati akimtambulisha balozi wa shule ya awali na msingi ya A plus iliyopo Kihonda Manispaa ya Morogoro,bi.Warda Makongwa ambae amesaini mkataba wa kuitangaza shule hiyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo,bwana Chomoka ambae ndie mkurugenzi wa shule hiyo,amesema ameamua kuanzisha shule hiyo ambayo ni ya mchepuo wa Kiingereza ili kusaidia jamii kupata elimu iliyobora inayoendana na mazingira ya kisasa.
Aidha amesema shule hiyo imejipanga vyema kuhakikisha watoto wanaosoma shuleni hapo wanalelewa katika misingi ya maadili ya Kitanzania na kwamba haitakuwa rahisi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijisia.
Kwa upande wake Bi.Warda Makongwa amesema kuwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto shuleni hapo.
Bi.Yasinta John ambae ni moja kati ya wazazi wenye watoto watatu wanaosoka katika hiyo akielezea akielezea utafauti wa shule hiyo na nyingine.