Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wajumbe, wanachama wa CCM na wakazi wa shina namba 7, Tawi la Wafugaji, Mtandika A, Kata ya Ruaha Mbuyuni ikiwa sehemu ya muendelezo ya ziara yake ya kuimarisha Chama pamoja na kukagua na kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Katibu Mkuu ameambatana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa shina namba 7, Tawi la Wafugaji, Mtandika A, Kata ya Ruaha Mbuyuni Ndugu Julius Leteo (kulia) kwa kusimamia vyema elimu ya Watoto wake.