….
Tarehe 28/5/2023 TETE FOUNDATION imeungana na jamii kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani, ambapo Taasisi hiyo imefanya maadhimisho hayo katika kituo na shule Amani iliyopo Mvomero – Mkoa wa Morogoro
Shule/ kituo cha Amani, ni kituo kinachojumuisha malezi ya kitaalam na kijamii Kwa Watoto Wanaoishi kwenye mazingira magumu, Uhitaji na wenye Ulemavu.
Ndani ya kituo hicho kuna Shule ya Msingi kuanzia darasa la awali Hadi darasa la saba na Shule ya Sekondari kuanzia kidato Cha kwanza hadi Cha Pili
Takwimu zinaonyesha kwamba mtoto wa kike anaeishi kwenye mazingira magumu, uhitaji na wenye ulemavu hukosa darasani siku 5 – 7 darasani kwa kukosa taulo za kike.
Katika maadhimisho hayo Mkurungezi wa TETE FOUNDATION, Bi. Suzana Senso amesema kutokana na takwimu hiyo, mwaka huu tumekuja na dhima “Sitakosa Shule Campaign” ambapo mwaka huu tumegawa taulo za kike za kutumia kwa muda wa miezi 6 kwa kila binti zaidi ya 50 waliopo kwenye shule ya Amani
Shukurani za kipekee kwa wadau walioshirikiana na TETE FOUNDATION kufanikisha hili zoezi ikiwemo UAP INSURANCE TANZANIA kwa kuwa sehemu ya kufanikisha zoezi hili bila kusahau wazalishaji wa taulo za kike za HQ PAD na Ministry ya “love of Christ Ministry” kwa kuwa sehemu ya kuhakikisha kila mtoto wa kike wa Shule ya Amani hakosi darasani kwa muda wa miezi 6 kutokana na kuwa kwenye hedhi
Asante kwa kuwa sehemu ya kurudisha tabasamu kwa mtoto wa kike.