Kamati maalum ya kupitia changamoto za kibiashara nchini iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 26 Mei imekutana na kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo J. Kidata ikiwa ni muendelezo wa kamati hiyo kupitia changamoto mbalimbali zinawakabili wafanyabiashara nchini na kupata mapendekezo ya namna bora ya kutatua changamoto hizo.
Kamati hiyo inoyongozwa na Mwenyekiti Dkt.John Jingu kwa siku mbili za tarehe 23 na 25 Mei, 2023 imekutana na Taasisi za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Bandari (TPA), Shirika la Viwango nchini (TBS) Pamoja na Tume ya Ushindani nchini (FCC) ili kupata kiini cha changamoto za kibiashara nchini kama zilivyoibuliwa na wafanyabishara katika kikao chao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kilichofanyika tarehe 17 Mei , 2023 Jijini Dar es Salaam.