Na Farida Sidy, Morogoro
Serikali Ya Awamu Ya Tano Imeendelea Kutoa Kipaumbele Katika Huduma Za Afya Kwa Wananchi Na Hivyo Kuchangia Katika Kukuza Uchumi Wa Taifa Ambapo Kati Ya Huduma Hizo Muhimu Ni Pamoja Na Upatikanaji Wa Chanjo Kwa Ajili Ya Kukinga Magonjwa Hususani Yanayowaathiri Watoto.
Kauli Hiyo Imetolewa Mkoani Morogoro Na Waziri Wa Afya Maendeleo Ya Jamii Jinsia Wazee Na Watoto Mh Ummy Mwalimu Alipokuwa Akizindua Kampeni Ya Chanjo Ya Surua Rubella Na Polio ambapo Kitaifa imefanyika Mkoani Humo, huku akiongeza kuwa, Mpaka Sasa Kupitia Wizara Ya Afya Chanjo Tisa Zinatolewa Tanzania Nzima.
Mhe Ummy Amesema Utaratibu Wa Chanjo Ya Surua Rubella Utaendelea Kutolewa Kwani Lengo La Kampeni Hii Ni Kuhakikisha Kila Mtoto Anapata Chanjo Huku Akitolea Ufafanuzi Wa Swali Lililoulizwa Kuwa Je Endapo Mtoto Alikwishapatiwa Chanjo,Kuna Ulazima Wa Kupata Chanjo?.
Nao Wadau Mbalimbali Wakiwemo Shirika La Afya Duniani Who Pamoja Na Shirika La Watoto Unicef Wameishukuru Serikali Kwa Ushirikiano Ambao Wanautoa Katika Sekta Ya Afya Na Kuahindi Kuendelea Na Jitihada Za Kutatua Changamoto Mbalimbali Katika Sekta Hiyo .
Kwa Upande Wa Wazazi Waliojitokeza Katika Chanjo Hiyo Wamesema Ni Muhimu Sana Kwa Watoto Kupata Chanjo Hivyo Kuwaasa Wazazi Wengine Nao Kujitokeza Kwa Ajili Ya Chanjo Kwa Kinga Ya Watoto Wao
Hata Hivyo Kauli Mbiu Ya Kampeni Ya Chanjo Ya Surua Rubella Kwa Mwaka 2019 Ni “Chanjo Ni Kinga Kwa Pamoja Tuwakinge “’.