Katika kuwafikia watu wengi zaidi na kutangaza shughuli mbalimbali za Bodi ya Filamu, tarehe 19 Mei, 2023 Bodi hiyo imesaini Hati ya Makubaliano na Waigizaji wakubwa nchini, Salim Ahmed (Gabo) na Jackline Wolper ya kuwa Mabalozi watakaokuwa na jukumu mama la kutangaza shughuli za Bodi hiyo pamoja na kuhamasisha masula mbalimbali ya Maendeleo ya Sekta ya Filamu nchini.
Kwa upande wake Bi. Jackline Wolper ameahidi kutumia nafasi ya ubalozi kwa kuifanya Bodi na shughuli zake kujulikana ndani na nje ya nchi kutokana na ushawishi wake kwenye jamii.
Aidha, Mabalozi hawa wanaungana na Balozi Yvonne Cherrie almaarufu Monalisa ambaye ameshakuwa Balozi wa Bodi ya Filamu kuanzia Mwaka 2022.