Makatibu wa afya kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakiwa ukumbini.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana akizungumza wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu wa afya Tanzania uliofanyika kitaifa Jijini Mwanza
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana, amewasisitiza Makatibu wa afya nchini kusimamia vyema mifumo ya ukusanyaji mapato kwenye maeneo yao ya kazi hatua itakayosaidia kuimarisha taasisi zao.
Ameyasema hayo leo Ijumaa Mei 19, 2023 wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Makatibu wa afya Tanzania ambao umefanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mkutano huo uliodumu kwa siku nne uliwakutanisha Makatibu wa afya zaidi ya 300 kutoka katika Mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Ameeleza kuwa kunaumuhimu Mkubwa wa kusimamia vizuri mifumo ili iweze kuongeza mapato yatakayosaidia kutekeleza majukumu mbalimbali.
” Ninaimani katika hizi siku nne mlizokuwa pamoja katika Mkutano wenu huu mtakuwa mmejengeana uwezo na uelewa mkubwa katika utendaji kazi wenu, hivyo endeleeni kufanya kazi kwa moyo na kwakujituma ili wananchi wazidi kupata huduma bora za afya, amesema Balandya
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu wa afya Bi.Juliana Mawala ametoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwanamna walivyowakarimu huku akiwaomba Makatibu hao kwenda kuongeza nguvu kazi zaidi katika kusimamia huduma kwa wananchi