Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akizugumza na mwananchi aliyefika katika Hospitali ya wilaya Kisarawe kwaajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Kisarawe wakati wa kambi maalum ya siku tatu ya matibabu inayofanyika wilayani humo.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Lisa Mageta akizungumza na diwani wa viti maalumu wa tarafa ya Sumn’gwi wilaya Kisarawe Valeriana Mkoka aliyefika katika hospitali ya wilaya Kisarawe kwaajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayotolewa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Kisarawe.
Wananchi wa wilaya ya Kisarawe wakisubiri kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya wilaya Kisarawe wakati wa kambi maalum ya siku tatu ya matibabu inayofanyika wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe.Fatma Nyangasa akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya wilaya hiyo kwajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tatu ya matibabu inayofanyika wilayani humo. (Picha na Khamisi Mussa).