Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda akiwasilisha mada kuhusu miundombinu ya DART katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusu DART inayofanyika kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.
Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda akionesha mchoro wa barabara za Mabasi yaedayo haraka zilizojengwa na zitakazojengwa jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kuhusu miundombinu ya DART katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusu DART inayofanyika kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.
Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda akifafanua jambo kwa washiriki wa semina wakati akiwasilisha mada kuhusu miundombinu ya DART katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusu DART inayofanyika kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.
Dkt. Eliphas Mollel Mkurugenzi Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala na Kaimu Mtendaji Mkuu DART kulia pamoja na washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa karibu wakati mada inayohusu ujenzi wa miundombinu ya DART ilipokuwaikiwasilishwa kwenye semina hiyo.
NA JOHN BUKUKU, DODOMA.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ipo katika mpango wa kutengeneza miundombinu ya barabara ya mabasi yaendayo haraka katika Mikoa inayokuwa kwa kasi ikiwemo Dodoma, Mwanza, Arusha pamoja na Tanga.
Akizungumza Mei 15, 2023 Jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya mabasi yaendayo haraka, Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda, amesema kuwa serikali inaendelea na juhudi kufikia Mikoa inayokuwa kwa kasi ili kufikisha huduma ya usafiri.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha inatengeneza mifumo ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka Mikoa yote ili kuhakikisha tunaondoa changamoto ya usafiri” amesema
Hata hivyo amebainisha kuwa kwa sasa wanaendelea na utekelezaji miradi katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mradi huo una awamu sita.
Amesema kuwa utekelezaji wa awamu ya kwanza tayari umemalizika, kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa awamu ya pili DART Mbagala ambapo umefikia asilimia 85.
“Mradi wa awamu ya tatu Gongo la Mboto tayari umeaza na umefika asilimia 10 katika utekelezaji wake” amesema.
Amefafanua kuwa awamu ya nne kutoka Tegeta kwenda mjini huku awamu ya tano utejengwa Ubungo.
“Awamu ya sita ni muendelezo wa mradi wa awamu kwanza na pili kutoka Mbagala rangi tatu hadi Vikindu, kutoka Kimara hadi Kibaha” amesema.
Ameeleza kuwa tayari fedha zote za utekelezaji wa miradi wa DART katika Mkoa wa Dar es Salaam zipo tayari lengo ni kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikia.
Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.
Jukumu kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa jiji la Dar es Salaam.
Malengo ya DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa ajili ya Dar es Salaam yatakayotumia jina la DART
Miongoni mwa malengo ni kuhakikisha kuna mtiririko bora wa usafiri kwenye mitaa na barabara za mjini, usimamizi wa wakala wenye ufanisi.