Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET),Dk Adolf Rutayuga akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na maonesho hayo.
………………
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha .RAIS wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi kwenye Maonesho ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi yatakayofanyika jijini Arusha .
Maonesho hayo yanaanza mei 16 hadi mei 22 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha huku kauli mbiu ikiwa ni ” elimu ya ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi kwa nguvu kazi mahiri ,ambapo washiriki zaidi 250 watashiriki katika maonyesho hayo .
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt Adolf Rutayuga amesema maonesho hayo yataanza hapo kesho na yatafunguliwa Rasmi mei 19 na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .
Ambapo amesema kuwa, kabla ya maonesho hayo kufunguliwa wataanza na kongamano litakalowashirikisha wadau zaidi ya 300.
Dkt Rutayuga ameeleza lengo la Maonesho hayo kuwa ni kuelezea umma vyuo vya ufundi stadi vinafanya nini , na kuonyesha maendeleo yaliyopo kwenye vyuo hivyo .
Aidha amebainisha kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia vijana wenye bunifu zao na kusaidia kuwaendeleza vijana wanaoshinda kwenye mashindano ya bunifu mbali mbali kwa lengo la kutoa motisha zaidi.
Amesema kuwa,maonesho hayo yatakwenda sambamba na Kongamano la siku mbili litakalofanyika mei 16 na mei 17 Jijini Arusha ambapo Mgeni Rasmi atakuwa ni Waziri wa kazi na ajira vijana na watu wenye ulemavu ,Prof Joyce Ndalichako.
Katika Kongamano hilo watajadili mada mbali mbali ikiwemo jinsi gani wanaweza kuwajengea umahiri vijana wanaosoma kwenye vyuo vya ufundi na walimu kukuza ujuzi walionao ili kuweza kuwafundisha vijana waweze kujiajiri.