Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na kamati ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).
Akizungumza na Wafanyabiasha leo tarehe 15/5/2023 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amesema kuwa tarehe 17/5/2023 kutakuwa na mkutano majira ya Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu MAGOGONI- ikulu.
“Viongozi wa Wafanyabiashara watakutana na Waziri Mkuu pamoja TRA Kwa ajili kumaliza changamoto iliyopo kwa njia ya mazungumzo” amesema Mhe. Makalla.
Hata hivyo amewasihi Wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.
Hata hivyo baadhi ya Wafanyabiashara bado wamegoma kufungua maduka.
Wafanyabiasha wamegoma kufanya biashara kwa kufunga maduka kuanzia leo tarehe 15.5.2023 kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo bandarini, kukamatwa kwa mizigo pamoja na uwepo wa sheria mpya usajili Stoo.
Imeelezwa kuwa dhamira ya kufanya mgomo huo wafanyabiashara wanahitaji uhuru wa biashara ili waweze kulipa kodi.