Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bugumangala ambapo tukio hilo lilitokea
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Bugumangala Kata ya Nyanguge wilayani Magu Mkoani Mwanza aliyefahamika kwa jina la Juliana Lukono, mwenye umri wa miaka 51 ameuawa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mihogo.
Akizungumza na wakazi wa Wilaya hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Willbroad Mutafungwa, amesema kuna mwanamama mmoja mkazi wa nyanguge ameokotwa akiwa amepoteza maisha lakini tukio lenyewe linaonyesha huyo mama ameuawa huku akieleza kuwa hayupo ambae atafanya tukio la kinyama namna hiyo kwenye mkoa wetu akabaki anatamba mtaani.
Aidha, Kamanda Mutafungwa ametangaza donge nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa wahusika waliofanya tukio hilo.
“Ndani ya siku saba kutoka leo jeshi la polisi litatoa zawadi kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa mtu au watu aliyefanya tukio hil la kihalifu tutatoa zawadi kwa huyo mtu shilingi milioni moja na laki tano,
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugumangala Paulo Julius, amewataka wakazi wa Kijiji hicho kuwa watulivu wakati uchunguzi wa jeshi la polisi ukiendelea.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa aliyefariki alikuwa ni mama yake mdogo na mimi nilipigiwa simu nikakuta amefariki.