Adeladius Makwega-MWANZA
Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya, ndugu Richard Mganga amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa watumishi kuwa wanachama wa bima mbalimbali maana inaweza kumsaidia kufikia na kuyafanikisha malengo mbalimbali katika maisha.
Kauli hiyo imetolewa Mei 12, 2023 wakati akifunga semina fupi ya hamasa kwa wafanyakazi wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya kujiunga na bima mbalimbali ambapo mawakala kadhaa wa bima walitembelea taasisi hiyo.
“Tumepata bahati ya ugeni kutoka Shirika la Bima la Taifa lenye wataalamu wazoefu, kama lilivyo shirika hilo, japokuwa yapo mashirika mengi ya bima kwa sasa, kwa kuwa hili ni shirika la umma lazima tuwaunge mkono.”
Wakishirika mafunzo hayo na hamasa ya kujiunga na bima mbalimbali, watumishi kadhaa baada ya semina hiyo walihamasika hadi kuuliza maswali juu ya bima hizo.
Swali la kwanza liliulizwa na Mohammed Mwiduchi ambaye ni Afisa Michezo Msaidizi, “Hapo umezungumzia kuhusiana na hasara yote, hapa gari linaangaliwa likiwa jipya tu, hapo ndipo litafidiwa kama gari la zamani hata kama umelipa bima kubwa imekuwa haifidiwi , kwa nini? “
Wakala wa Bima ndugu Florian Kagombe akasema kuwa, Bima kubwa ya gari lazima ukate kwa gari jipya ambalo ndiyo kwanza limeingia nchini au limesajiriwa miaka mitano tangu lilipoingianchini.
“Sidhani kwa sasa kama unanunua gari leo hii litapewa namba ya A , sasa tupo namba E, kama utalipia gari ambalo ni la zamani itakuwa si sahihi, itambulike kuwa Bima Kubwa ni hiari lakini Bima Ndogo ni ya lazima.
Gari jipya likipata ajali linafidiwa na kweli inatambulika kuwa umepoteza na umepata hasara, kwa gari la zamani hilo hata kama mteja atakuwa tayari
ameshapata pesa kiasi, ifahamike wazi bima inalipa bahari mbaya tu.”
Semina hiyo iliendelea na mtumishi mwingine aliyepata nafasi ya kuuliza swali ni Jerome Sellungato ambaye ni dereva, yeye akija na hoja ya thamani ya chombo kilichopata ajali, kama mthamini akifanya kazi yake na mwenye chombo akapinga tathmini hiyo, Je nani atautatua utata huo?
“Kwanza ni mkaguzi, pili ni Bima yenyewe na tatu mahakama.”
Ndani ya semina hiyo watumishi hao wa umma walipata nafasi ya kutambua maana ya neno akiba ambapo ni kitu unachokiweka kukisaidie baadaye na lazima iwe na malengo. Huku pia semina hiyo ikitaja aina sita za bima nazo ni; Elimu, Malengo, Matumaini, Majaliwa, Ndoa na
Kustaafu.