Wahitimu wa mafunzo ya ufundi VETA wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa benki ya KCB.
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza katika mahafali ya vijana 150 waliohitimu katika.chuo hicho waliofadhiliwa na benki ya KCB kwa kushirikiana na serikali ya maendeleo ya Ujerumani (GIZ)
……
Julieth Laizer, Arusha
Arusha.MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewashauri vijana wanaohitimu vyuo vya ufundi kutumia mitandao ya kijamii kujifunza teknolojia mpya badala ya kutumia mitandao hiyo kupoteza muda.
Akihutubia vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi (VETA)ya muda mfupi yaliyofadhiliwa na Shirika la maendeleo la Ujerumani(GIZ) Kwa kushirikiana na Benki ya KCB Mongela amesema vijana Wana uwezo mkubwa wa kujifunza teknolojia mpya kwenye mitandao ya kijamii.
“Vijana tunatumia muda mwingi sana kwenye simu mjiulize mnapata nini kwenye hizo simu, tumieni muda mwingi kujifunza ujuzi mpya teknolojia zinaingia Kila siku hivyo kupitia hizi simu za mkononi mnaweza kuwa mafundi wa kisasa zaidi”amesema Mongela.
Amesema mafundi wengi hufanya kazi bila uaminifu hivyo kupelekea kuwepo msemo usemao Fundi wa uhakika ni kinyozi peke yake kutokana na kutofanya kazi Kwa uaminifu .
“Ikitokea umepewa kazi Fanya kama mtaalamu Hadi aliyekupatia kazi aseme Fundi ni huyu siwezi kutumia Fundi mwingine msije mkaendeleza huu usemi wa mtaani kuwa Fundi mzuri ni kinyozi tu”amesema.
Naye mkuu wa Idara ya masoko,uhusiano na mawasiliano Benki ya KCB Christina Manyenye amesema katika program hiyo waliandikisha vijana 150 na walifanikiwa kuhitimu vijana 146 katika ufundi wa Mabomba,Ujenzi na Umeme wa majumbani.
Amesema lengo la programu hiyo ni kuinua uchumi wa watanzania hivyo walitoa nafasi hiyo Kwa vijana wa kitanzania ambapo wamefadhili sehemu Mbalimbali mbali ikiwemo Arusha Zanzibar.
Ametoa wito Kwa vijana kutumia Elimu ya ufundi waliyoipata kubadilisha Jamii huku akiwataka kuwa mfano wa kuigwa ambapo alisema Wanatarajia kufadhili vijana zaidi 5000 kupitia programu hiyo.
“Mpaka Sasa takribani watu 1880 wamenufaika na pragramu hii, lakini tulimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa tutawafadhili vijana zaidi ya 5000 hivyo mwezi wa sita wataingia wengine vyuoni”amesema Manyenye.