Norwegian Church Aid Tanzania pamoja na washirika wamezindua msafara wa vijana, kisiwani Pemba kuhamasisha Amani na Utengemano wa jamii, wenye ujumbe ‘’ Amani Yetu, Kesho Yangu’’. Msafara huo utapita katika Wilaya nne ikiwemo Chake Chake, Mkoani, Wete na Micheweni ( Nizar Seleman Utanga (Afisa Uchechemuza na Mawasiliano – NCA-Tanzania
Msafara wa vijana wenye ujumbe “Amani Yetu, Kesho Yangu’’ unawaleta pamoja mabalozi wa amani, vijana, wanaume, wanawake, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wawakilishi toka asasi za kiraia
Msafara huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Utengamano wa jamii unaotekelezwa Zanzibar na Pemba tangu mwaka 2020. Mradi huo unatekelezwa na Norwegian Church Aid kwa kushirikiana na Zanzibar Interfaith Centre/Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani (KKKT DMP) na Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa ufadhili kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
Kupitia mpango huu, mafunzo mbalimbali yamewezeshwa yakiwalenga vijana, wanawake, wasichana na viongozi wa dini ili kuimarisha uwezo wao katika kujenga amani na kuimarisha mahusiano ya dini mbalimbali. Aidha, nyenzo mbalimbali zimeendelea kutumika ikiwemo utenzi, michezo, maigizo na ngonjera ili kuongeza vionjo na kufikisha ujumbe kwa jamii.
Timu za Amani za wilaya ya Wete na Micheweni zikichuana kuwania kombe la Interfaith Amani 2023 lililoandawaliwa na shirika la Makanisa Norway kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Tanzania
.………………………………
Mkoani, Pemba, 8 Mai 2023
Leo Mkoani,Pemba, NCA Tanzania pamoja na washirika wetu tunayofuraha kuzindua msafara wa vijana kuhamasisha amani na utengemano wa jamii ‘’ amani yetu, kesho yangu’’ katika Wilaya nne, ikiwemo Chake Chake, Mkoani, Wete na Micheweni tarehe 8 mpaka 10 Mai 2023.
Msafara wa vijana kuhamasisha amani na utengemano wa jamii ‘’ Amani Yetu, Kesho Yangu’’ unawaleta pamoja mabalozi wa amani vijana, vikundi vidogo za fedha, wanaume, wanawake, vijana, taasisi za , dini , viongozi wa dini, viongozi wa serikali, vyombo vya habari na asasi za kiraia kutoka Pemba.
Malengo; – viongozi wa dini na vijana waliowezeshwa na wameimarisha mshikamano wa kijamii na amani endelevu, Vijana waliojipanga na kushiriki kikamilifu ili kukuza amani na uwiano wa kijamii, ushirikishwajwi nyanja za kitaifa na kikanda za kujenga amani na kuhamasisha wanawake na vijana kujiunga na kilimo kinachostahamili mabadiliko tabianchi ilikueweza kujiondoka kwenye lindi la umasikini.
Msafara huo wa vijana utaanzia Kusini kuelekea Kaskazini Pemba katika Wilaya 4 ambazo ni Wilaya ya Wete, Micheweni, Chakechacke, Mkoani ambapo yatafanyika mashindano ya michezo ya kiwilaya ‘’Interfaith Amani Cup 2023’’.
Msafara huo wa amani ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Utengamani wa Kijamii -Zanzibar na Tanzania Bara ilioyoanza 2020. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Msaada wa Makanisa ya Norway (Norwegian Church Aid) kwa kushirikiana na Zanzibar Interfaith Centre (ZANZIC)/Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania i, Dayosisi ya Masharik na Pwani (KKKT DMP) na Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania. Eneo linalolengwa ni Pemba na Unguja, lenye uhusiano na Tanzania Bara na Kanda ya Afrika Mashariki.
Kupitia mpango huu, programu inawezesha mafunzo kwa mabalozi wa vijana, kuwezesha matukio ya michezo na matukio ya maigizo kwa vijana ili kubadilishana uzoefu na kusambaza taarifa za kustahamiliana na kuvumiliana miongoni mwa dini mbalimbali na kuishi pamoja.
Ili kukuza uelewa zaidi na kuthamini amani na mshikamano wa kijamii, NCA na watendaji wa imani wataendeleza kazi nzuri ya kamati za dini mbalimbali, mabalozi wa amani wa vijana, wazalishaji wa kilimo kwa kubadilishana mbinu bora na hadithi za mafanikio kupitia mashairi, kaswida, hadithi za mabadiliko ya hati kutoka kwa walengwa hadi. kuvutia na kujihusisha na jumuiya pana ili kushiriki na kuendeleza uelewa mpana zaidi juu ya kulinda amani.
Mpango huu unachangia ukamilishaji wa mpango endelevu SGD:1-Hakuna umaskini, 2-Usalama wa Chakula na Lishe, 3-Ubora wa afya na ustawi ,8 – Ajira stahiki na Maisha bora, 10 – Kupambania usawa, 16: Ujenzi wa taasisi imara yenye Amani na usawa
NCA ilisajiliwa kama shirika lisilokuwa la kiserikali nchini tokea mwaka 2006, likiwa na makao yake makuu jijini Dar es Sa-laam. Tangu wakati huo, tumejenga ushirikiano imara na kulea asasi za dini mbalimbali ili kufanya kazi pamoja kwa ajili ya: Kuwawezesha wananchi waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umasiki na kushiriki kikamilifu katika jamii, kujenga jamii jumuishi na zenye amani ili watanzania wote waishi na kuheshimu utu wa mwanadamu. Vipaumbele vya shirika la NCA nchini Tanzania ni Usawa wa Kijamii, Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, Kuimarisha taasisi za kidini, huduma za afya endelevu inazotolewa na asasi za kidini.
Kauli mbiu hitakayotumika katika msafara huu ni “ Amani yangu,Kesho Yetu”