Mradi huo ulikamilika Aprili 20, 2023 na STAMIGOLD kuanza rasmi kutumia umeme wa gridiyaTaifa Aprili 26, 2023.
Njia ya umeme iliyojengwa ni ya ukubwa wa kilovoti 33.
Njia hiyo una umbali wa kilometa 105 kutoka kituo cha kupokea umeme cha Mpomvu – Geita.
Ujenzi umehusisha njia ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD.
Kituo hicho kimejengwa kwa transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 10 kila moja, na transfoma mbili za MVA 2.5
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo ACP. Advera Bulimba ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza Wilayani humo kutokana na uwepo umeme wa uhakika.