Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde wakifuatilia michango ya wabunge walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara hiyo leo tarehe 09/05/2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde wakifuatilia michango ya wabunge walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara hiyo leo tarehe 09/05/2023 jijini Dodoma.
…………………..
Wakulima wapata 3,050,621 nchini wamesajiliwa katika mfumo wa kidigitali ampapo kati yao 801, 776 wamenufaika na mpango wa ruzuku ya mbolea kwenye mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2023/2024 Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, serikali imewatambua wakulima walionufaika na mbolea ya ruzuku kwa majina yao kamili, mahali walipo, aina ya mazao na ukubwa wa mashamba na maeneo yao wanayofanyia shughuli za kilimo.
Aidha Waziri wa Kiimo amesema serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) itaendelea na zoezi la kusajili wakulima na kutoa kadi lengo ikiwa ni kuwasajili wakulima 7,000, 000 ifikapo 2025.
” Zoezi hili litaunganisha kanzidata na satelite, taarifa za afya ya udongo kwa kila mkulima na huduma za ugani ili Taifa liweze kuwa na uhakika wa takwimu za wakulima”, alisema Waziri Bashe.
Amesema waingizaji wakubwa wa mbolea 28, mawakala wadogo, 3, 265 na wazalishaji wa ndani watatu (3) wamesajiliwa katika mfumo wa ruzuku ya mbolea ili kuhakikisha kuwa usambazaji wa mbolea unafanikiwa.