Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya CHRISTINA MUSYANI – ACP
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa kufanya operesheni, misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa hali inayopelekea Amani na Utulivu kuendelea kuwepo.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MUSA PWELE [47] Mkazi wa Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuzini na maharimu. Tukio hili limetokea Mei 05, 2023 Jijini Mbeya baada ya mtuhumiwa kumtishia binti yake wa kumzaa kuwa hatampatia huduma ikiwepo mahitaji ya shule na huduma nyinginezo na kutokana na mashinikizo hayo alifanikiwa kumbaka mtoto wake huyo.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwani uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo ni mjamzito.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuendelea kupeana elimu ili baadhi ya watu wenye tabia ya kufanya vitendo vya ukatili wa kingono ambao unasababisha athari za kimwili na kisaikolijia kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Aidha Jeshi la Polisi linaimeza jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kukemea vitendo vya ukatili wa
kijinsia na kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya vitendo hivyo ili hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo kuzuia kutotendeka pamoja na kuwachukulia hatua wahusika.
Imetolewa na:
CHRISTINA MUSYANI – ACP
Kaimu Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.