Mkuu wa mkoa wa Mara Meja jenerali Suleiman Mzee ametoa siku 3 kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Kukarabati miundombinu ya standi ya Msusoma katika eneo la Bweri endapo watashindwa kuanza nakukamilisha kwa wakati ukaratabati huo atazuia wafanya biashara wanaotumia standi hiyo kulipa ushuru.
Pia Mkuu wa mkoa Meja jenerali Suleiman mzee amesikitishwa na Usimamizi wa standi hiyo licha ya wafanya biashara kulipa fedha zao kwaajili ya usafi hakuna chochote kinacjofanyika katika eneo hilo
“nimesikitishwa na ubovu wa standi hii uwepo wa chafu katika eneo hili hata Usimamizi tu hauridhishi kabisa Kama mtashindwa kuanza kwa wakati nakumaliza nitazuia watu wasilipe ushuru wa hapa haiwezekani hatutavumiliana kwa mambo kama haya”Meja jenerali Suleiman Mzee Rc Mara.
Wakizungumza baadhi ya wafanya biashara akiwemo maria mwita kwaniba ya wafanya biashara wengine wamesema wanasikitishwa na mazingira ya standi hiyo kwani haina hadhi ya stand kutokana na mkoa huo ambao ametoka Baba wa Taifa haunananani na mazingira mengine.
“Huu mkoa wa muasisi wa Taifa hili ukiangalia standi haifanani kabisa tunalipishwa fedha za uendeshaji lakini umejaa uchafu kila pahala tukuombe mkuu wa mkoa ulismamie hili”Mariam Mwita Mfanya Biashara wea standi ya Mabasi Manispaa ya Musoma.