Meneja wa Kampuni ya Napol inayojihusisa na uchenjuaji wa dhahabu Mcharo Zuberi akimuelezea Joseph Issack mwananchi alietembelea banda lao namna wanavyofanya kazi na wachimbaji wadogo wadogo kwenye maonesho ya madini yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.
…..
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Kampuni ya Napol Mining Limited iliyoko Geita inayojihusisha na uchenjuaji wa dhahabu imeiomba Serikali iwawezeshe kupata maeneo ya machimbo kutokana na sehemu nyingi kuchukuliwa na baadhi ya wawekezaji wakubwa hali inayopeleka wachimbaji wadogo wadogo kushindwa kupata fursa ya maeneo ya kuchimba.
Ombi hilo limetolewa leo Jumatatu Mei 8, 2024 na Meneja wa Napol Mcharo Zuberi, wakati akizungumza na Fullshangwe Blog kwenye maonesho ya madini yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.
Amesema wachimbaji wadogo wadogo watakapokuwa wamepata maeneo yao ya kuchimba itawasaidia kujikwamua kiuchumi hatua itakayosaidia kuongeza pato la taifa.
Aidha ameeleza kuwa baadhi ya vihusika vya uchenjuaji wa dhahabu ikiwemo Sayanaidi, Naitiriki na Safyuriki vinabei kubwa hivyo kupelekea zoezi la uchenjuaji kupata hasara, tunaomba Serikali iangalie utaratibu wa kutupunguzia bei hizo ili tuweze kufanya kazi hiyo kwa tija.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Kampuni ya Mimina Bw.Scallion Tegamaisho, amewashauri vijaa wanaotoka vyuoni kuamini rasilimali za Tanzania zilizopo zinatosha kama mtaji wa kuwapa ajira na wakaweza kujiajiri wenye.
“Mnapo maliza masomo msisubili kuajiriwa kunavitu vingi sana vya kufanya hapa nchini, Mimi ni mchimbaji na nimeenda mbali zaidi kwa ajili ya kuyapa madini thamani niliweza kuchimba jiwe la doromite linalochimbwa kwenye ukanda wa Pwani na Tanga baada ya hapo nalisaga na kutengeneza rangi maalumu kwaajili ya kumalizia ukarabati wa majengo.